![]() |
Liverpool |
Timu ya
Stoke City, ikiwa uwanja wa nyumbani wa Britannia, walizinduka toka kufungwa
Bao la Penati la Sekunde 35 iliyofungwa na Nahodha Steven Gerrard na kuwatandika
Liverpool bao 3-1.
Aidha magoli
mbili ya wachezaji Jon Walters na la Kenwyne Jones ndio yamewapa Stoke City
ushindi wao wa kwanza katika Mechi 4 na kuendeleza wimbi lao la kutofungwa
katika Mechi 9 ikiwa na pamoja ya kutofungwa Uwanjani kwao tangu Februari Mwaka
huu.
Kipigo cha
Liverpool katika Dimba la Britannia
kimeendeleza Rekodi yao ya kutoshinda hapo na pia kuwarudisha hadi nafasi ya 10
wakiwa Pointi 8 nyuma ya Timu iliyokamata nafasi ya 4.
![]() |
Manchester City |
Nao Mabingwa
watetezi wa Ligi kuu soka Uingereza
Manchester City ambao wako nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi hiyo ,
walijikuta wakichapwaa Bao 1-0 na Sunderland huko uwanja wa Stadium of Light, kwa goli la
Mchezaji wao wa zamani Adam Johnson na
hivyo kuwafanya wawe Pointi 7
nyuma ya vinara Manchester United ambao
nao walijituma na kuwafunga Newcastle Bao 4-3
wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wa
Old Trafford kwa Bao la ushindi kufungwa Dakika ya 90 na Chicharito huku
Chelsea wakiitungua Norwich City kwa Bao 1-0 na kujizatiti nafasi ya 3 wakiwa
Pointi 4 nyuma ya Manchester City huku wakiwa na Mechi 1 mkononi.
![]() |
Gareth Bale |
Aston Villa
wakicheza na Tottenham wamekubali kulizwa bao 4-0 , ikiwemo Hetitriki ya Gareth
Bale na kuwapa ushindi Tottenham huo 4-0
dhidi ya Aston Villa waliokuwa kwao Villa Park na hicho kuwa kipigo chao cha
pili kizito baada ya kutandikwa 8-0 na Chelsea majuzi.
MATOKEO:
Jumatano 26
Desemba 2012
Everton 2
Wigan 1
Fulham 1
Southampton 1
![]() |
Man United |
Man United 4
Newcastle 3
Norwich 0
Chelsea 1
QPR 1 West
Brom 2
Reading 0
Swansea 0
Sunderland 1
Man City 2
Aston Villa
4 Tottenham 0
Stoke 3
Liverpool 1
MECHI
ZIJAZO:
Jumamosi 29
Desemba 2012
[SAA 9 Dak
45 Mchana]
Sunderland v
Tottenham
[SAA 12
Jioni]
Aston Villa
v Wigan
Fulham v
Swansea
Man United v
West Brom
Norwich v
Man City
Reading v
West Ham
Stoke v
Southampton
[SAA 2 na
Nusu Usiku]
Arsenal v
Newcastle
Jumapili 30
Desemba 2012
[SAA 10 na
Nusu Jioni]
Everton v
Chelsea
[SAA 1
Usiku]
QPR v
Liverpool
1 | Manchester United | 19 | Point 46 |
2 | Manchester City | 19 | Point 39 |
3 | Chelsea | 18 | Point 35 |
4 | Tottenham | 19 | Point 33 |
5 | Everton | 19 | Point 33 |
6 | West Bromwich | 19 | Point 33 |
7 | Arsenal | 18 | Point 30 |
8 | Stoke | 19 | Point 28 |
9 | Swansea City | 19 | Point 25 |
10 | Liverpool | 19 | Point 25 |
11 | Norwich City | 19 | Point 25 |
12 | West Ham | 18 | Point 23 |
13 | Sunderland | 19 | Point 22 |
14 | Fulham | 19 | Point 21 |
15 | Newcastle | 19 | Point 20 |
16 | Aston Villa | 19 | Point 18 |
17 | Southampton | 18 | Point 16 |
18 | Wigan Athletic | 19 | Point 15 |
19 | Reading | 19 | Point 10 |
20 | QPR | 19 | Point 10 |
No comments:
Post a Comment