Chipolopolo yala mweleka kwa Taifa Stars . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, December 23, 2012

Chipolopolo yala mweleka kwa Taifa Stars .


Mashabiki wa timu ya Taifa Stars
wakishagilia mara baada
ya Mrisho Ngasa
kufungo goli la kwanza
dhidi ya Chipolopolo .
Bao la ushindi lilifungwa na Mrisho Ngassa katika Dakika ya 44 baada ya kupokea krosi safi kutoka kwa Mwinyi Kazimoto limeipa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ushindi dhidi ya mabingwa wa Afika timu ya taifa ya Zambia katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.



Timu zote ambazo zilikuwa zimewakosa wachezaji wao muhimu ziliuanza mchezo wa vizuri huku Taifa Stars wanaofundishwa na kocha  Kim Poulsen wakionekana kucheza vizuri kwenye upande wa ulinzi na safu ya kiungo iliyokuwa chini ya  Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Isaac Domayo na Sure Boy.

 


Mchezaji wa Taifa Stars Mrisho Ngasa akishangilia na kupongezwa na wenzake mara baada ya kufunga goli la mkwanza katika mchezo huo.


Mashabiki wa timu ya Taifa Stars wakishagilia mara baada ya Mrisho Ngasa kufungo goli la kwanza dhidi ya Chipolopolo katika mchezo huo.


Mashabiki wa timu ya taifa ya Zambia wakishangilia timu yao katika mchezo huo.



ZAMBIA: Danny Munyao,

 Chintu Kampamba,

 Hichani Himonde,

Chisamba Lungu,

James Chamanga,

Moses Phiri,

Christopher Katongo,

Felix Katongo,

 Nathan Sinkala,

Rodrick Kabwe,

 Isaac Chansa.
Zambia ama Chipolopolo  chini ya Kocha Bora Afrika Herve Renard, Kipindi cha Pili, walirudi kwa kasi  lakini wakiwa na mchezaji bora wa Afrika wa BBC Chris Katongo ,Hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa matokeo yakiwa 1-0  hivyo Taifa  Stars  kutoka na ushindi mzuri ikiupata  kwa kucheza soka safi kabisa la kuridhisha. 












Makocha wa Zambia wakitoka uwanjani baada ya mechi kumalizika.


Kulia ni Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu nchini Zambia Kalusha Bwalya na mabalozi wa Zambia nchini Judith Kangoma-Kapijimpanga na Balozi Tanzania nchini Zambia Bi. Grace Mujumi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mchezo huo.



TAIFA STARS: Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Kevin Yondan, Frank Domayo, Salum Abubakar, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Mrisho Ngassa, Khamis Mcha.

  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad