Kituo cha
Polisi kata ya Mugoma
wilayani Ngara
mkoani Kagera
kikiwa kimechomwa
moto.
|
Waendesha
mashitaka wa Jeshi la Polisi Hamisa Mataka na Tumaini Membi, wamewataja washitakiwa
kuwa ni Method John ambaye ni afisa Mtendaji
wa kijiji cha Mugoma, Suleimu Zuberi, Rashid Ally, Issa Athumani, Simon Chuma
na Aman Maulid.
Amesema watu
hao wanatuhumiwa kuwaua Koplo Paschal na Konstebo Alexandar, ambao walikuwa
waajiriwa wa jeshi la polisi Tanzania, katika tukio lililotokea Desemba 15
mwaka huu majira ya saa 8 mchana, katika eneo la Mugoma.
Katika
shitaka la pili, watu hao wanashitakiwa kwa kosa la kuchoma moto kituo cha
polisi cha Mugoma, na kusababisha hasara yenye thamani ya zaidi shilingi
milioni 68, kutokana na uharibifu wa mali mbalimbali za jeshi hilo.
Washitakiwa
hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa walikuwa mbele ya mlinzi wa Amani Bw.
Andrew Kabuka, na pia mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji,
ambapo wamerudishwa rumande hadi January 3 mwaka kesho.
Chanzo:Radio
Kwizera FM.
No comments:
Post a Comment