Mwanamuziki wa Bongo Fleva Ray C amemtembelea Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam na kumshukuru kwa msaada wa matibabu kipindi alipokuwa mgonjwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, December 10, 2012

Mwanamuziki wa Bongo Fleva Ray C amemtembelea Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam na kumshukuru kwa msaada wa matibabu kipindi alipokuwa mgonjwa.

Rais  Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mwanamuziki Rehema Chalamila aka Ray C leo(Desemba 12,2012) Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati mwanamuziki huyo alipoenda kumtembelea Rais  na kumpa shukrani kwa kumsaidia kwenye matibabu ya juu ya ugonjwa uliokuwa ukimsumbua.


Aidha Ray C alimueleza Rais kwamba afya yake imeimarika na kwamba muda mfupi ujao atarudi kuendelea na kazi yake ya muziki. 



Kwa upande wa mama yake Ray C amemshukuru Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanae kwa kugharamia matibabu yote ya mwanae.




Raisi Jakaya Kikwete akiwa pamoja na Ray C, Mama yake mzazi Ray C - Margreth Mtweve na aliyevaa nguo za pinki upande wa kulia ni dada yake Ray C - Sarah Mtweve. (Picha na Freddy Maro)
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad