Kardinali
Rugambwa alizaliwa Julai 12,1912 ambapo mazishi hayo ni kumbukumbu muhimu kwa
Watanzania na Waafrika kwa ujumla.
Historia
ya Kardinali Rugambwa, alipewa Upadre mwaka 1943, Uaskofu 1952, Ukardinali mwaka 1960 ambapo
mwaka 1969 akawa Askofu Mkuu Jimbo la Dar es Salaam hadi alipostaafu mwaka
1992.
Kardinali
Rugambwa alianzisha Kanisa Kuu Jimbo la Bukoba, kuleta Seminari Kuu ya Ntungamo
na kujenga Shule ya Sekondari Rugambwa.
Pia
alifanikisha ujenzi wa Hospitali ya Mugana, kuanzisha VIKOBA kwenye Parokia,
Seminari Ndogo ya Visiga na Seminari Kuu ya Segerea iliyoko Dar es Salaam.
Kardinali
Rugambwa alifariki Desemba 1997 ambapo Kardinali
Rugambwa alizaliwa Kijiji cha Bukongo, Parokia ya Rutabo, Kata ya Kamachunu,
Wilaya ya Muleba, mkoani Kagera akitokea katika familia iliyotukuka ya
kitawala.
Alipata
elimu ya Sekondari katika Shule ya Seminari Rubya Junior na kujiunga katika
Semiri Kuu ya Katigondo, nchini Uganda, ambako alihitimu masomo ya Falsafa na
Theolojia, Desemba 12, 1943.
|
No comments:
Post a Comment