Kampuni ya Bia Tanzania kupitia Bia ya Kilimanjaro Premium Lager hatimaye yakabidhi mabasi mapya ya kisasa kwa timu za Simba na Yanga. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, September 21, 2012

Kampuni ya Bia Tanzania kupitia Bia ya Kilimanjaro Premium Lager hatimaye yakabidhi mabasi mapya ya kisasa kwa timu za Simba na Yanga.



Mkurugenzi wa TBL, Robin Goetzche akimkabidhi Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage nyaraka za basi la timu hiyo lililokabidhiwa leo makao makuu ya TBL Ilala kama sehemu ya ufadhili wa Kilimanjaro Premium Lager kwa Klabu ya Simba.


Makamu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga akipokea nyaraka za kukubali makabidhiano ya basi la Klabu hiyo toka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania Robin Goetzche leo.




Mabasi mawili ya kisasa ambayo yamekabidhiwa kwa Klabu za Simba na Yanga yakiwa yameegeshwa katika viwanja vya aofisi za Kampuni ya Bia Tanzania kabla hayajabandikwa nembo za Kilimanjaro Premium Lager na za klabu husika tayari kwa hafla ya makabidhiano  leo Ijumaa TBL Ilala.


Mashabiki wa Yanga wakilizindua basi lao na Msafara wa Yanga nao ukiondoka TBL Ilala utaelekea katika Tawi la Ubungo katika kituo cha mabasi na kuelekea katika Tawi la Manzese, Lango la Jiji Magomeni, Buguruni, Mwembe Yanga, Mtoni kwa Aziz Ali, Mkombozi na hatimaye kumalizia katika makao makuu ya Jangwani, Kariakoo.


Mashabiki wa Simba wakilizindua basi lao na Msafara wa timu ya Simba ukiondoka TBL Ilala utaelekea katika Tawi la Vuvuzela lililopo Makao Makuu ya klabu hiyo Kariakoo Mtaa wa Msimbazi kisha utaelekea katika Tawi la Magomeni Mpira Pesa, Ubungo katika kituo cha mabasi na hatimaye Tawi la Wailes Temeke.


Mashabiki.


Popote ukikatiza usafiri huu basi fahamu mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati wapo njiani.


Ukiliona hili mtaani tambua mnyama mkali wekundu wa Msimbazi Simba  anakatiza.


Aidha Kilimanjaro Premium Lager imedhamini klabu hizi hivi tangu mwaka 2008.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad