 |
Mabasi
mawili ya kisasa ambayo yatakabidhiwa kwa Klabu za Simba na Yanga yakiwa
yameegeshwa katika viwanja vya aofisi za Kampuni ya Bia Tanzania kabla
hayajabandikwa nembo za Kilimanjaro Premium Lager na za klabu husika tayari kwa
hafla ya makabidhiano Ijumaa TBL Ilala.
|
Ligi Kuu Vodacom septemba 19, 2012,
imeendelea kwa Yanga kutandikwa bao 3-0 huko Morogoro mikononi mwa Mtibwa Sugar
wakati Jijini Dar es Salaam Mabingwa watetezi Simba wakiendeleza wimbi la
ushindi kwa kuichapa JKT Ruvu bao 2-0.
 |
Huko Morogoro, Mtibwa Sugar walipata ushindi
wao wa 3-0 dhidi ya Yanga kwa bao za
Dickson Daudi, Dakika ya 11, na bao mbili za Juma Javu za Dakika za 45 na 77.
Dakika ya 90
Yanga wakapata penati lakini Hamis Kiiza akashindwa kufunga na mwamuzi akapuliz
kipenga cha kuashiria mwisho wa mchezo.
Hii ni Mechi ya pili kwa Yanga na hadi sasa
hawajaambua ushindi na walitoka sare 0-0 na Tanzania Prisons katika Mechi yao
ya kwanza.
|
 |
Nao mabingwa watetezi wa ligi hiyo ya Vodacom
Tanzania bara Wekundu wa Msimbazi, Simba wakicheza bila ya mshambuliaji wao
tegemeo Emmanuel Okwi kutolewa nje kwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza cha
mchezo, walipata ushindi wa bao 2-0
dhidi ya Maafande wa JKT Ruvu kwa mabao ya kiungo Amri Kiemba aliyefunga bao la
kwanza na Haruna Moshi Boban aliyepiga la pili.
Kufuatia matokeo hayo Simba inaendelea
kukamata usukani mwa ligi kwa kukusanya pointi 6, magoli matano ya kufunga na
wakiwa hawajuruhusu nyvu zao kuguswa.
Simba walishinda mechi ya kwanza ya ligi kwa
3 - 0 dhidi ya African Lyon.
|
Huko Mwanza, wenyeji Toto African walitoka
sare 2-2 na Azam FC huku Toto wakisawazisha bao katika Dakika ya 90 mfungaji
akiwa Maganga na Mussa Saidi ili hali magoli ya wana lamba lamba Azam FC yakifungwa
na Abdulhalim Homoud na Kipre Tchetche .
 |
Tanzania Prisons ya Mbeya ikiwa nyumbani Sokoine wametoka sare ya bao 1 - 1 na Coastal Union ya Tanga,
Kagera Sugar wametoka sare tasa na JKT Oljoro, huku Ruvu Shooting wakiifunga
Mgambo JKT 2-1.
|
Aidha Ratiba ya Ligi kuu Vodacom
Tanzania bara itaendelea tena kwa Mechi zijazo:
Septemba 22 .
Yanga v JKT Ruvu
[National Stadium, Dar Es Salaam].
Azam v Mtibwa Sugar [Azam Complex,
Dar es Salaam]
JKT Oljoro v Polisi Morogoro [Sheikh
Amri Abeid, Arusha]
Coastal Union v Toto Africans
[Mkwakwani, Tanga]
Septemba
23.
Mgambo JKT v Kagera Sugar[Mkwakwani,
Tanga]
Simba Ruvu v Shootings [National
Stadium, Dar Es Salaam]
African Lyon v Tanzania Prisons
[Azam Complex, Dar es Salaam]
No comments:
Post a Comment