Katika maandamano ya Kulaani mauaji ya Daudi Mwangosi Leo ,Wana habari waitaka Serikali kuchukua hatua na damu ya Mwangosi iwe shule kwao. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, September 11, 2012

Katika maandamano ya Kulaani mauaji ya Daudi Mwangosi Leo ,Wana habari waitaka Serikali kuchukua hatua na damu ya Mwangosi iwe shule kwao.


Wanahabari wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati wa maandamano hayo leo wameandamana kutoka Kituo Cha Televisheni cha Channel Ten na kuhitimisha maaandamano yao katika Viwanja vya Jangwani kwa ajili ya kulaani mauji ya kikatili aliyofanyiwa mwandishi mwenzao  Daudi Mwangosi wa Kituo cha Chanel Ten mkoni Iringa.


Katika Maandamo hayo Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emannuel Nchimbi alifika Viwanja vya Jangwani kupokea maandano hayo lakini alitimuliwa na wanahabari.

(PICHA NA GPL).



Na hii ndio taswira ya Wazir. Nchimbi alipokuwa akitolewa maeneo ya jangwani jijini Dar es salaam baada ya wana habari kumgomea asiongee lolote katika maandamano yao.

Hatua hiyo imetokea baaada ya waziri huyo wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi kufika katika viwanja vya jangwani kwa ajili ya kujipa jukumu la kupokea maandamano bila mwaliko.



Kutokana na zomea zomea hiyo ya wanahabari hao dhidi ya waziri NCHIMBI hali ilionekana kuwa si shwari na kupelekea waziri huyo kuondolewa na Rais wa UTPC Keneth Simbaya na viongozi wengine wakiwemo askari polisi.
 


Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania Nevil Meena akitoa Tamko katika  maandamano hayo"Kuna watu wanahoji tunaandamana alafu iweje wakati siye ndio wenye vyombo vya habari si tuandike tu?
Hapana kuandamana kwetu kunamaana sana tumeandamana sikama hatuna uwezo wakufanya kitu zaidi ya kuandamana, tunazo silaha kubwa zaidi ya maandamano lakini hii ni hatuayapili baada ya matamko mbalimbali kutolewa.


Aidha meena akahoji hivyo inakuaje kama sikumoja watu wakaamka wakakuta hakuna chombo chochote cha habari kilicho hewani hakuna tv, hakuna radio na wala hakuna magazeti nchi hii itakuwaje?


Wanahabari waendelee kuwa na utulivu hatua mbalimbali zitakazoendelea kuchukuliwa watafahamishwa kuhusiana na tukio hilo."


Vingozi wengi wa vyama vya waandishi wa habari waliotoa maoni yao kwenye mkusanyiko huo waliitaka serikali wachukue hatua na damu ya Mwangosi iwe shule kwao.



Wazee wa Feva nao hawakua nyuma kufatilia Maandamano hayo.


Waandishi wakiigiza tukio la mauaji ya Daudi Mwangosi namna lilivyotokea huko Iringa wakati wa maandamanoyao yalioanzia kwenye ofisi za Chanel ten hadi jangwani leo asubuhi.


Na hii ndio picha ambayo inaonyesha mwili wa Mwana habari Daudi Mwangosi ukiwa umedhurika vibaya huku pembeni yake akiwa askari wa FFU akiwa hoi ingawa haijafahamika alikuwa hoi kwa hilo bomu linalosadikiwa kumuua Daudi au ni  bahati mbaya.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad