Cheka
alimpiga Nyilawila katika raundi ya sita ya pambano hilo lililokuwa la uzani wa
Super Middle la raundi 12 lililofanyika kwenye ukumbi wa PTA, Temeke jijini Dar
es Salaam na kutwaa ubingwa wa Mabara wa UBO uliokuwa wazi.
Pambano hilo
lililohudhuriwa na mashabiki lukuki, lilishuhudia raundi zote tano za kwanza
Nyilawila akionyesha kumdhibiti Cheka kwa kumchezea 'kibabe' akitumia nguvu
nyingi kujihami na baadhi ya watu ukumbini kuamini mwisho wa tambo za Cheka
zilikuwa zimewadia.
Hata hivyo
raudni ya sita ilipoanza Cheka alionyesha amebadilika na hasa baada ya kocha
wake Abdallahj Saleh 'Komando' kupanda ulingoni na kuzungumza na bondia huyo na
kumshushia kipigo Nyilawila, ambapo moja ya makonde matatu ya mfululizo
yalimpeleka chini mpinzani wake.
Mwamuzi wa
pambano hilo Jerome Waluza alimhesabia Nyilawila ambaye alijitahidi kuinuka lakini ghafla akaonyesha ishara kwamba
asingeweza kuendelea na pambano hilo na ukumbi mzima kuripuka kwa shangwe
akishangiliwa Cheka ambaye hiyo ni mara ya pili kumpiga Nyilawila.
Kabla ya
pambano hilo lililoanza majira ya saa 3;40 usiku, kulikuwa na mapambano saba ya
utangulizi pamoja na burudani ya muziki toka bendi ya Mashujaa ambao hata hivyo
sio wapenzi wengi walioweza kuishuhudia kutokana na kuondoka ukumbini mapema.
Katika
pambano la kwanza la utangulizi Said Mbelwa alimpiga kwa pointi Dickson
Mwakipesile, Juma Kihiyo alipigwa kwa pointi na Ibrahim Mahokola katika pambano
lililovutia kwa namna mabondia hao walivyoonyeshana kazi.
Bondia
Karama Nyilawila (kulia) akijitahidi kukwepa makonde ya mpinzani wake Francis
Cheka wakati wa mpambano wao uliofanyika jana usiku.
|
Pia mdogo wa
Cheka, Cosmas Cheka alifanikiwa kuibuka na ushindi wa pointi dhidi ya Fadhil
Awadh katika pamnbano jingine lililosisimua wengi kwa ufundi uliokuwa
ukionyesha na mabondia hao, naye Shaaban Kilumbelumbe alimpiga kwa pointi
Anthony Mathias kabla ya Safari Mbiyu kumpiga kwa KO ya raundi ya kwanza
Khalfan Jumanne.
Michezo
minginme iliwakutanisha Stan Kessy na Seba Temba, pambano lililoisha kwa
mabondia hao kutoka sare na Hassani Kidebe alitolewa nishai na Deo Samwel kwa
kupigwa kwa pointi.
Mgeni rasmi
katika pambano hilo alikuwa Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam
ambaye aliutangazia umma kwamba kama Mlezi wa Ngumi za Kulipwa amefanikiwa
kuwafuta wafadhili katika mchezo huo na kumtambulisha raia mmoja wa kigeni
kwamba ni miongoni mwao.
Refarii wa
mpambano akiwaelekeza mabondia wasicheze kwa kukumbatiana
|
Mabondia
Karama Nyilawila kushoto na Fransic Cheka wakionesheana umwamba wa kutupiana
makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi katika ukumbi wa
PTA Sabasaba Cheka alishinda kwa K,o raundi ya sita picha na www.superdboxingcoach.
|
No comments:
Post a Comment