Serikali yatoa wito kwa wananchi tutotegemea wawekezaji kutoka nje kwa kila Jambo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, September 12, 2012

Serikali yatoa wito kwa wananchi tutotegemea wawekezaji kutoka nje kwa kila Jambo.

Na:Augustine Mgendi.



TARIME.


Serikali  imesema kuwa kamwe haiwezi kumtegemea mwekezaji  kwa kila kitu huku baadhi ya Mambo yanaweza kufanywa na wanajamiii wenyewe katika sehemu huska.


Kauli hiyo ya Serikali ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime Bw John Henjewele katika hafla ya kukabidhi Madawati kwa baadhi ya shule zinazozunguka mgodi wa ABG North Mara, Vifaa vya Shule kwa baadhi ya wanafunzi na baiskel ya Magurudumu matatu kwa watu watatu wasiojiweza.


Alisema kuwa pamoja na Misaada inayotolewa na Mgodi huo kwa Jamii lakini pia serikali inashukuru Mahusiano Mazuri yaliyopo katika Mgodi huo wa ABG North Mara na Jamii.



 “Kwanza tushukuru sana Mahusiano yaliyopo kati ya Mgodi huu na Jamii lakini pia hatuwezi kumtegemea Mwekezaji kwa kila Jambo lazima sisi wenyewe tujitoe katika kufanikisha baadhi ya Mambo yetu” alisema Mkuu huyo wa wilaya.

Aidha  Meneja mkuu wa Mgodi wa North Mara Bw Gary Chapman,amesema Mgodi huo ni miongoni mwa Migodi Afrika ambayo imekuwa ikiwekeza katika Jamii hasa katika suala la Elimu,Afya,Maji na Maendeleo katika Jamii.


Mkuu huyo wa Wilaya  aliushukuru Mgodi huo kwa kugundua hali ya Walemavu,kutoa vifaa vya Elimu huku akisema hiyo ni hatua moja mbele katika kuisaidia Jamii.



Amesema Pamoja na kutotimiza mahitaji kwa shule za Sekondary kwa asilimia mia lakini watajitahidi kushirikiana na Jamii jiyo katika kujiletea Maendeleo.


 “Mgodi huu ni moja ya Mgodi Afrika ambao unajitolea katika kusaidia Jamii hasa katika Elimu,afya,maji na Masuala la Maendeleo,lakini pamoja na kutotimiza Mahitaji ya Jamii kwa asilimia kubwa bado tutaendelea kushirikia na nao” alisema Bw Gary Chapman.


 
Watu waliopewa Baiskel hizo za Miguu mitatu ni pamoja na  Eliza Mwikwabe ambaye ni mfanyabiashara ndogondogo,Penina Mseti muuza mboga na Nyanya pamoja na Gesongo Chacha ambaye ni fundi wa kuchomelea vyuma.

 

Awali akisoma Risala kwa Mgeni Rasmi Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Nyangoto Bw Ghati Keraryo amesema kuwa shule zote mbili za Nyangoto na Matare  zina jumla ya Madawati 202 kati ya 654 ambayo yanahitajika na kwamba bado shule hizo zina upungufu wa Viti 46 na meza 18.


Mbali na Msaada huo wa Madawati kwa shule hizo,Mwalimu Ghati Keraryo ameuomba  Mgodi huo kuendelea kujenga Shule hizo kama Mkataba ulivyoainisha kati  ya Kijiji na Mgodi.


Amesema kwa niaba ya Walimu wa shule hizo wanapenda kutoa shukurani kwa Mgodi wa ABG North Mara kwa kutambua Umuhimu wa Changamoto moja wapo zinazokabili shule hizo ikizingatiwa kwamba shule hizo zipo karibu na Mgodi huo.


Uongozi wa Mgodi huo umetoa Madawati zaidi ya 1000 kwa shule za Nyangoto na Matare zilizopo katika eneo la Nyamongo wilayani Tarime Mkoani Mara huku Miradi yote Mitatu ya Elimu ambayo ni msaada wa baiskeli na Madawati hayo vikigharimu kiasi cha shilingi milioni 188.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad