Polisi jamii yafika fainali ngazi ya Tarafa wilayani Ngara huku timu ya Kabanga FC ikiibuka Bingwa tarafa ya Kanazi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, September 14, 2012

Polisi jamii yafika fainali ngazi ya Tarafa wilayani Ngara huku timu ya Kabanga FC ikiibuka Bingwa tarafa ya Kanazi.


Wachezaji wa timu ya Kabanga FC  ya kata ya Kabanga   wilayani  Ngara mkoani  Kagera  wakiwa na nyuso za tabasamu  baada ya kuifunga timu ya Matunda Fc bao 3-1 katika Michuano ya polisi jamii Ngazi ya tarafa  ya kanazi wilayani humo .



Timu hiyo  ilipata zawadi ya Beberu la mbuzi lenye thamani ya shilingi elfu 40 , fedha taslimu elfu 50  pamoja na jozi moja ya jezi  huku Matunda FC  wakiambulia  shilingi elfu 50 na mpira mmoja  licha ya kuwa na washabiki lukuki waliobeba matunda aina mbalimbali siku hiyo.



Aidha Kamanda wa polisi mkoani Kagera (RPC) Philipo Karangi alikuwa  mgeni rasmi katia fainali hiyo ambapo Timu hizo zitaungana na timu sita toka tarafa za Nyamiaga, Rulenge na Murusagamba  katika michuano ya polisi jamii ngazi ya wilaya na kupata Bingwa wa mashindano hayo wa  wilaya itakayochuana na wilaya nyingine mkoani Kagera.




Imeandikwa  Na :Shaaban Ndyamukama  NGARA.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad