Kwa mwenendo huu, Askofu Severine Niwemugizi awataka watanzania kuliombea taifa ili lipate viongozi wanaojali utu na maisha ya mtanzania. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, September 14, 2012

Kwa mwenendo huu, Askofu Severine Niwemugizi awataka watanzania kuliombea taifa ili lipate viongozi wanaojali utu na maisha ya mtanzania.


Maskini mwenzangu huyu, hata hajui kitu zaidi ya kisu chake na muhogo na akimaliza hapo ana enda  kuiuza huko mtaani ikiwa imechemka. Hakuna  shule, huduma na  mapenzi mazuri.


Hawa nao wameenda mahali ambapo wanadanganyishiwa kuwa ni shule, lakini je, kiuhalisia, hapo ni shule? Hao ni wanafunzi kweli?

Hawa wanafundishwa kuwa wanasiasa. Je, wanapewa ujuzi wa  uzalendo au ni mwanasiasa tu bora siasa?



Huku maisha ni burudani kabisaaaaa. Na kando hapo kuna wazazi wanapiga makofi na kuwatuza kabisaaaaa. Haya, huyu siku amekuwa mbunge, pale mjengoni patakalika kweli?


....na hapa ndipo watu wanapojifunza maisha  ni nini/ hawa ndiyo  wataweza kuyamudu maisha yoyote yale na pia kujua ugumu na uzuri wa maisha ...Nchi hii inahitaji maombezi ya kiulimwengu zaidi maana sisi wenyewe naamini imetushinda kabisa.
Mungu ibariki Tanzania
Wabariki na Watanzania wake.


Aidha Askofu wa jimbo katoliki la Rulenge Ngara  Severine Niwemugizi amewataka watanzania kuungana kwa pamoja kuliombea taifa ili lipate viongozi wanaojali utu na maisha ya mtanzania.



 Akizungumza katika mkutano mkuu wa shirika la moyo mtakatifu wa yesu mjini Biharamulo ,Askofu Niwemugizi amesema taifa limeanza kuelekea pabaya kutokana na viongozi wasiojali utu na maisha ya watanzania.


 Amesema Tuyafanyayo mengi bado ni mambo ya hovyo hovyo, na wenye kuongoza kuyafanya hayo ya hovyo hovyo ni viongozi wetu.

Askofu Niwemugizi  amesema wapo baadhi ya viongozi waliopewa madaraka kuwaongoza wananchi na kuwaletea maendeleo ambao badala yake wanawanyonya wananchi kwa kuweka mbele maslahi binafsi.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad