Ligi kuu Tanzania bara Yanga na Prisons,Simba na Africa Lyon hapo kesho huku Ulaya Arsenal v Southampton, Manchester United v Wigan Athletic, Bayern Munich v Mainz,Borussia Dortmund v Bayer Leverkusen, Getafe v Barcelona, Sevilla v Real Madrid na AC Milan v Atalanta Bergamo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, September 14, 2012

Ligi kuu Tanzania bara Yanga na Prisons,Simba na Africa Lyon hapo kesho huku Ulaya Arsenal v Southampton, Manchester United v Wigan Athletic, Bayern Munich v Mainz,Borussia Dortmund v Bayer Leverkusen, Getafe v Barcelona, Sevilla v Real Madrid na AC Milan v Atalanta Bergamo.

 Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara 2012/2013 inaanza kutimua vumbi kesho (Septemba 15 mwaka huu) ambapo timu zote 14 zitakuwa kwenye viwanja saba tofauti.



Mabingwa watetezi Simba wataikaribisha African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 


Mjini Morogoro, Polisi Dodoma watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri wakati jijini Tanga, Mgambo JKT ambayo imepanda daraja msimu huu itaumana na Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani.


Tanzania Prisons ambayo nayo imerejea Ligi kuu VPL msimu huu itaialika Yanga kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya ili hali  JKT Ruvu na Ruvu Shooting zitapambana kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam huku Azam ikiwatembelea Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Katiba.


Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Toto Africans dhidi ya Oljoro JKT


Mechi zote zitaanza saa 10.30 jioni.


Viingilio katika mechi ya Simba na African Lyon vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani na bluu, sh. 8,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 viti vya VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 20,000. 


Viingilio kwa mechi nyingine vitakuwa sh. 3,000 na sh. 10,000.

 BAADA MAPUMZIKO WIKI 2 BPL, LA LIGA, SERIE A, BUNDESLIGA KULINDIMA DIMBANI!


 Aidha Wikiendi hii, baada ya ‘mapumziko’ ya Wiki mbili kupisha Mechi za Kimataifa, Wadau kila pembe ya Dunia watarudia tena kupata burudani yao ya kawaida ya kushabikia Klabu zao kwa kufaidi uhondo wa Ligi kubwa Barani Ulaya na watafunguliwa pazia Ijumaa Usiku kwa Mechi ya Bundesliga kati ya FC Augsburg v VfL Wolfsburg na Jumamosi kufuata nyingine za Ligi Kuu Uingereza, La Liga na Serie A huku Wiki ijayo, Jumanne, Jumatano na Alhamisi, kitaanza kitimtim cha Michuano mikubwa ya Klabu Ulaya, UEFA CHAMPIONZ LIGI na EUROPA LIGI kwa hatua za Makundi.


Ligi kuu soka Uingereza

Jumamosi Septemba 15
[Saa 8 Dak 45 Mchana]

Norwich City v West Ham United

[Saa 11 Jioni]

Arsenal v Southampton

Aston Villa v Swansea City

Fulham v West Bromwich Albion

Manchester United v Wigan Athletic

Queens Park Rangers v Chelsea

Stoke City v Manchester City

[Saa 1 na Nusu Usiku]

Sunderland v Liverpool

Jumapili September 16
[Saa 12 Jioni]

Reading v Tottenham Hotspur

Jumatatu Septemba 17
[Saa 4 Usiku]

Everton v Newcastle United

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Ligi kuu soka Ujerumani

Ijumaa Septemba 14
[Saa 3 na Nusu Usiku]

FC Augsburg v VfL Wolfsburg

Jumamosi Septemba 15
[Saa 10 na Nusu Jioni]

Bayern Munich v Mainz

Borussia Dortmund v Bayer Leverkusen

Borussia Moenchengladbach v Nuremberg

Hanover 96 v Werder Bremen

VfB Stuttgart v Fortuna Duesseldorf

[Saa 1 na Nusu Usiku]

Greuther Fuerth v Schalke 04

Jumapili Septemba 16

[Saa 10 na Nusu Jioni]

Freiburg v Hoffenheim

Eintracht Frankfurt v Hamburg SV

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Ligi kuu soka Hispania 

Jumamosi Septemba 15
[Saa 11 Jioni]

Malaga v Levante

[Saa 1 Usiku] 

Valencia v Celta Vigo

[Saa 3 Usiku] 

Getafe v Barcelona

[Saa 5 Usiku] 

Sevilla v Real Madrid

Jumapili Septemba 16

[Saa 7 Mchana]

Espanyol v Athletic Bilbao

[Saa 11 Jioni]

Granada CF v Deportivo Coruna

[Saa 1 Usiku] 

Osasuna v Real Mallorca

[Saa 2 Dak 50 Usiku] 

Real Sociedad v Real Zaragoza

[Saa 4 na Nusu Usiku] 

Atletico Madrid v Rayo Vallecano

Jumatatu Septemba 17

[Saa 4 na Nusu Usiku] 

Real Valladolid v Real Betis

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Ligi kuu soka Italia.

Jumamosi Septemba 15
[Saa 1 Usiku] 

Palermo v Cagliari

[Saa 3 Dak 45 Usiku] 

AC Milan v Atalanta Bergamo

Jumapili Septemba 16

[Saa 7 na Nusu Mchana] 

Chievo Verona v Lazio

[Saa 10 Jioni Usiku] 

AS Roma v Bologna

Fiorentina v Catania

Genoa v Juventus

Napoli v Parma

Pescara v Sampdoria

Siena v Udinese

[Saa 3 Dak 45 Usiku] 

Torino v Inter Milan






No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad