Hudson Bagege ndiye mshindi wa nafasi ya Uenyekiti Chama cha Mapinduzi Wilayani Ngara mkoani Kagera akimshinda Bi Helena Adrian aliyeshindwa kuitetea nafasi yake kwa kura 489. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, September 30, 2012

Hudson Bagege ndiye mshindi wa nafasi ya Uenyekiti Chama cha Mapinduzi Wilayani Ngara mkoani Kagera akimshinda Bi Helena Adrian aliyeshindwa kuitetea nafasi yake kwa kura 489.

Chama cha mapinduzi CCM wilayani Ngara mkoani Kagera kimepata viongozi wapya kufuatia uchaguzi uliofanyika jana ambapo aliyekuwa mwenyekiti wake Bi Helena Adrian ameshindwa kuitetea nafasi yake .




Msimamizi wa uchaguzi huo Kaptein Mstaafu Daud Salum Kateme amemtangaza Bw Hudson Bagege kuwa mshindi wa nafasi ya Uenyekiti baada ya kupata kura 489 dhidi ya 257 za Bi Helena Adrian.


Aidha Bw Issa Samma amechaguliwa kuwa mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM, NEC baada ya kupata kura 664 dhidi ya 111 alizopata Bi Helena Adrian huku Bi Ernestina Mpinzile akipata kura 6.


Katika mkutano huo  Bw Damian Godard amechaguliwa kuwa katibu wa itikadi na uenzi wa CCM katika wilaya ya Ngara baada ya kupata kura 83  na kuwahsinda Bw Georgia Myonyera na Erick Niramachumu.


Wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa ni Bw Said Sudy,Bw  Mkiza Byamungu, Bw Stanlasus Batakanwa, Bi Ninian Bakari na Bw Rehema Ramadhan.


Aidha huko Jijini Mwanza aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi  Bw Lawrence Masha ameshinda uchaguzi wa mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM,  NEC kuwakilisha wilaya ya Nyamagana jijini Mwnaza .


Bw Masha amewashinda wapinzani wake, Bw Biku Kotecha na Bw James Bwire katika uchaguzi wa mjumbe wa NEC  uliofanyika jana. 


Katika uchaguzi huo Kada wa siku nyingi wa CCM, Bw Raphael Shilatu amewashinda Bw Yahya Nyaonge, Bw Joseph Bupamba na Bw Mashaka Kaguna.

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad