Mapato na matokeo ya Ligi kuu soka Tanzania bara pamoja na matokeo ya Ligi kuu soka Zanzibar msimu wa 2012/2013. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, September 17, 2012

Mapato na matokeo ya Ligi kuu soka Tanzania bara pamoja na matokeo ya Ligi kuu soka Zanzibar msimu wa 2012/2013.

Ligi Kuu Bara, rasmi kama Vodacom Premier League, VPL, ilianza kwa timu zote 14 kushuka katika viwanja saba kuwania ubingwa wa Msimu mpya wa Mwaka 2012/13 na Mabingwa watetezi Simba walianza vyema kwa ushindi wa bao 3-0 dhidi ya African  Lyon, Timu iliyoshika nafasi ya Pili Azam FC ikashinda  bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar na Vigogo Yanga kubanwa mbavu kwa sare ya 0-0 huko Mbeya walipocheza na timu ya maafande wa Magereza ya Prisons.



Mabingwa watetezi, Simba, waliaanza utetezi kwa kuwa nyumbani kucheza na African Lyon, Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na bao za Emmanel Okwi, Mrisho Ngassa na Daniel Akuffo ziliwapa ushindi wa bao 3-0.

Huko Kaitaba, Mkoani Kagera, Timu iliyoshika nafasi ya Pili Msimu uliopita, Azam FC, iliidunga Kagera Sugar bao 1-0 kwa bao la Abdulahalim Humoud la Dakika ya 57.


Yanga, ambao walikuwa nafasi ya 3, Msimu uliopita wwalitoka sare huko Mbeya Uwanja wa Sokoine ya 0-0 na Tanzania Prisons.


 MATOKEO-Septemba 15.

Simba 3 African Lyon 0

Polisi Morogoro 0 Mtibwa Sugar Sugar 0

Tanzania Prisons 0 Yanga 0

Mgambo 0 Coastal Union 1

JKT Ruvu 2 Ruvu Shootings 1

Kagera Sugar 0 Azam 1

Toto Africans 1 JKT Oljoro 1

Ratiba MECHI ZIJAZO:
Septemba 19

JKT Ruvu v Simba [National Stadium, Dar Es Salaam]
Mtibwa Sugar Sugar v Yanga [Jamuhuri, Morogoro]
African Lyon v Polisi Morogoro [[Azam Complex, Dar es Salaam]]]
Ruvu Shootings v Mgambo JKT [[Mabatini, Pwani], Pwani]
Tanzania Prisons v Coastal Union [Sokoine, Mbeya]
Kagera Sugarv JKT Oljoro  [Kaitaba, Kagera]
Toto Africans v Azam [CCM Kirumba, Mwanza]



Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Simba na African Lyon iliyochezwa jana (Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 67,793,000.


Washabiki 11,505 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Kila timu ilipata sh. 14,603,263.47 wakati asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyokatwa ni sh. 10,341,305.08.


Mgawo mwingine umekwenda kwa msimamizi wa kituo sh. 20,000, posho ya kamishna wa mechi sh. 114,000, mwamuzi wa akiba sh. 70,000, et iti.sh. 3,175,000, vishina kwenye tiketi (attachments) sh. 345,150, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.


Umeme sh. 300,000, ulinzi na usafi uwanjani sh. 2,350,000, Kamati ya Ligi sh. 4,867,754.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,920,652.69, uwanja sh. 4,867,754.49, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,947,101.86, gharama za mchezo sh. 4,867,754.49.


Nayo mechi ya ligi hiyo kati ya Tanzania Prisons na Yanga iliyochezwa jana (Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya imeingiza sh. 50,435,000.


Aidha watazamaji 112 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya JKT Ruvu na Ruvu Shooting iliyofanyika jana (Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.


Mapato yaliyopatikana katika mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 3,000 na sh. 10,000 ni 340,000. Mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; kila timu sh. 29,465.87, asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 51,864.40, maandalizi ya uwanja sh. 100,000 na tiketi sh. 89,916.


Kamati ya Ligi sh. 9,821.95, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 5,893.17, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 3,928.78, gharama za mchezo sh. 9,821.95 na uwanja sh. 9,821.95.




Huko nako katika Ligi Kuu ya Zanzibar maarufu Zanzibar Grand Malt Premier League imeendelea  katika Viwanja viwili tofauti ambapo Kisiwani Unguja, Klabu ya Bandari walicheza na Mafunzo na mechi hiyo imemalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Katika muendelezo wa ligi hiyi hiyo huko Kisiwani Pemba Klabu ya Jamhuri ambao ni Wawakilishi wa Zanzibar katika michuano ya Kimataifa wakiwa na tiketi ya kushiriki katika Kombe la Shirikisho walicheza na Chipukizi na kuanza kuonja machungu ya ligi baada ya kukubali kipigo cha bao 3-0.


Mabao ya Chipukizi yalifungwa na Muhsin Mohammed katika dakika ya 11 ya kipndi cha kwanza, bao la pili likifungwa na Faki Maalim katika dakika ya 21 ya kipindi cha kwanza na mpaka mapumziko Chipukizi walikuwa wakiongoza kwa mabao 2-0.


Kipindi cha pili kilianza kwa Jamhuri kutaka kusawazisha, huku Chipukizi wakitaka kuongeza, alikuwa ni Faki Maalim kwa mara nyengine tena aliyeifungia Chipukizi bao la 3 katika dakika ya 60, na hadi dakika 90 zinamalizika za mchezo huo, Chipukizi 3 Jamhuri 0.


Ligi hiyo inatarajia kuendelea tena kesho kwa mechi moja katika uwanja wa Amaan kwa kuzikutanisha timu za Mtende Rangers na Chuoni.

RATIBA:


Jumatatu Septemba 17
 
Mtende v Chuoni [Amaan, Unguja]

Jumanne Septemba 18

Zimamoto v Mundu [Amaan, Unguja]

Jumamosi Septemba 22

KMKM v Bandari [Amaan, Unguja]
Super Falcon v Jamhuri [Gombani, Pemba]

Jumapili Septemba 23

Mafunzo v Malindi [Amaan, Unguja]
Chipukizi v Duma [Gombani, Pemba]

Jumatatu Septemba 24

Mtende v Mundu [Amaan, Unguja]

Jumanne Septemba 25

Zimamoto v Chuoni [Amaan, Unguja]


TIMU 12 ZINAZOSHIRIKI:

TOKA UNGUJA:

-Bandari
-Chuoni
TOKA PEMBA:

-Chipukizi
-Duma
-Jamhuri
-Super Falcon
-KMKM
-Mafunzo
-Malindi
-Mundu
-Mtende
Zimamoto
 





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad