Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemuita ikulu
mwanamuziki anayefanya vizuri kwa sasa kwenye Bongo Fleva, Nasibu Abdul Jumaa
‘Diamond Platnumz’ na kumpa jukumu maalum.
Kwa
mujibu wa Diamond, Rais Kikwete alimwita ikulu Magogoni, Dar es Salaam
na kumpa shavu la kwenda kufanya shoo kwenye mkutano maalum utakaofanyika
Washington DC nchini Marekani hivi karibuni.
“Yaa,
rais aliniita akaniambia kuna shoo natakiwa kwenda kufanya Marekani.
“Kwa
mara ya kwanza nitasafiri nje ya nchi na madensa wangu wanne na msemaji mmoja.
Sasa hivi hawataki kutembea na kupanda magari wasije wakakosa hiyo safari,”
alisema Diamond na kuongeza kuwa baada ya kuumwa, mawazo aliyaweka kwenye
mchongo huo hivyo mambo mengine yataendelea ikiwa ni pamoja na kufanya kolabo
na mwanamuziki wa kimataifa wa Nigeria, J. Martins.![]() |
|
Aidha
kupitia Show ya Mkasi ya wiki imetufanya
tufahamu mambo 10 muhimu tusiyoyajua kutoka kwa Diamond kama ifuatavyo:
1.
Yupo kwenye mazungumzo na label moja kubwa duniani ambao walimtafuta baada ya
kufanya show ya Big Brother Africa.
2.Ana
simu nne na moja ina line mbili, hivyo ana line tano.Simu yake huiweka silent
muda wote kwakuwa zinapigwa muda mwingi. Anayo moja maalum ambayo watu wengi
hawaijui.
3.
Ana nyimbo 133 ambazo ameshazirekodi tayari.
4.Mama
yake alikuwa anampeleka kwenye talent show na kumsubiria hadi usiku mpaka
aperform ndo wanarudi wote. Ndugu zake wengine waliona anamdekeza mwanae.
5.Zamani
alikuwa anapenda kurap lakini aliona ukirap huwezi kupata mademu. Alipokuwa
akiimba watu wengi walikuwa wanamkataza kwakuwa waliona hawezi.
6.
Q Chilla ndiye msanii anayempenda zaidi na muda mwingi husikiliza nyimbo zake.
7.
Anamaliza mjengo wake uliopo Tegeta Dar es Salaam.
8.Anapenda
kuja kuwa kama Usher Raymond.
9.Anapenda
jinsi Dully anawasupport wasanii wachanga kwa kuwashauri na kuwapa moyo kuliko
wasanii wengine wakongwe ndo maana anasema huwa hachuji.
10.Maproducer
anaowazimia Tanzania Manecky, KGT, Manwalter na Marco Chali.
|







No comments:
Post a Comment