Tazama matukio makubwa na muhimu Jumatatu hii kiuchumi abiria zaidi ya 400 wakwama Mpanda ,kisiasa PICHA ZA VURUGU MOROGORO na kimichezo Yanga na Luka Modric aondoka Tottenham kwenda Real Madrid. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, August 27, 2012

Tazama matukio makubwa na muhimu Jumatatu hii kiuchumi abiria zaidi ya 400 wakwama Mpanda ,kisiasa PICHA ZA VURUGU MOROGORO na kimichezo Yanga na Luka Modric aondoka Tottenham kwenda Real Madrid.


Abiria waliokuwa wanasafiri na treni wakiwa wanasubilia msaada wa injini nyingine ya treni baada ya kunusurika kifo kufuatia treni waliokuwa wanasafiria kupata ajali baada ya behewa namba 3366 kuacha njia muda mfupi baada ya kuondoka katika kituo cha mpanda, ajali hiyo ilitokea jana saa 3 usiku katika eneo la Tambukareri, abiria zaidi ya 400 hadi sasa wamekwama wakisubiri kufanyika kwa utaratibu mwingine. (Picha na Walter Mguluchuma)
Blogzamikoa


Tottenham imetangaza kuwa wamekubali Uhamisho wa Kiungo wao Luka Modric kwenda Real Madrid kwa Ada inayokisiwa kuwa ni Pauni Milioni 30 na hivyo kumaliza mvutano wa muda mrefu kati ya Mchezaji huyo na Klabu yake.

Uthibitisho wa Uhamisho wa Mchezaji huyo wa Kimataifa kutoka Croatia umetolewa kwenye Tovuti ya Tottenham ambako Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Daniel Levy huku na Rais wa Real Madrid, Florentino Perez, ambae ameelezea furaha yake na kumkaribisha Modric huko Madrid.


Mbali ya makubaliano ya Uhamisho huu wa Modric, Klabu hizo mbili pia zimetiliana saini Mkataba wa kuanzisha Ushirika kati yao utakaohusisha Wachezaji, Makocha na Biashara.


Luka Modric alihamia Spurs Mwaka 2008 kutoka Dinamo Zagreb na kuichezea Spurs Mechi 160 na kufunga Mabao 17.


Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati Yanga jana ilimaliza ziara yao huko Kigali, Rwanda kwa kuifunga Police FC bao 2 - 1  huku  Yanga wakiifunga Rayon Sports bao 2-0 katika Mechi iliyochezwa Uwanja wa Amahoro huko Kigali, Rwanda kwa bao za Hamisi Kiiza na Simon Msuva.

Mbali ya Yanga kucheza Mechi hizo za Kirafiki huko Rwanda, Msafara wa Mabingwa hao wa Kagame Cup, wakiongozwa na Mwenyekiti wao Yussuf Manji na Mama Fatma Karume walimtembelea Rais wa Nchi hiyo Paul Kagame.

Yanga imeondoka Kigali leo asubuhi kurejea Nchini Tanzania.



Mkuu wa wilaya  ya Nkasi  Bw. Idd Kimanta akiangua kilio  wakati  akisikitikia  na kuona uchungu  juu ya utendaji mbaya  wa Mkurugenzi  na wakuu wa idara w  halmashauri hiyo  mbele ya baraza la madiwani  mjini Namanyere kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nkasi  Bi. Saada Mwaruka.

Moshi wa mabomu yaliolipuliwa kutawanya maandamano ya chadema leo mjini Morogoro.


 Wafuasi wa chadema wakiwa na maandamao hayo mjini morogoro


Aidha Mtu mmoja anadai kupoteza maisha katika mapambano hayo yaliyoibuka mapema leo mjini Morogoro baina ya Jeshi la polisi mkoani humo na wafuasi wa Cahdema.

Ujumbe uliopatikana kwenye mtandao wa Facebook kutoka kwa Zitto Kabwe umeeleza kufariki kwa mtu huyo.

Jeshi la polisi limetumia mabomu ya machozi kukabiliana na wafuasi wa chama cha CHADEMA, wanaoshinikiza kuandamana kuelekea kwenye mkutano wao unaofanyika Uwanja wa Ndege.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad