Ligi kuu soka Uingereza Arsenal tena 0 - 0 huku Liverpool v/s Man City 2 – 2. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, August 26, 2012

Ligi kuu soka Uingereza Arsenal tena 0 - 0 huku Liverpool v/s Man City 2 – 2.


Makosa ya Mabeki wa Liverpool mwishoni mwa mchezo leo yametoa mwanya kwa Mabingwa watetezi Manchester City kutoka sare ya bao 2-2 Uwanjani Anfield katika Mechi ya Ligi Kuu Uingereza  na kuendeleza ile rekodi yao ya kutoishinda Liverpool Uwanjani hapo toka Mwaka 2003.


MAGOLI:
Liverpool

-34 Martin Skrtel
-66 Luis Suarez.

Man City

-63 Yaya Toure
-80 Carlos Teve.
 
Hadi mapumziko Liverpool walikuwa wakiongoza kwa bao 1-0. Lakini Man City wakapiga bao la pili na kuifanya Mechi imalizike sare ya 2-2 baada ya pasi mbovu ya kurudisha nyuma ya Martin Skrtel kunaswa na Carlos Tevez aliefunga.

Stoke 0-0 Arsenal



Kwa mara ya pili mfululizo washika Mitutu wa London  Arsenal wametoka sare ya 0-0 na  kwenye Uwanjani Britannia na timu ya  Stoke City katika Mechi ya Ligi Kuu licha ya kuitawala Mechi yote, Aslimia 67 kwa 33, kupata Kona 11 kwa 0, kupiga Shuti 17 kwa 6 lakini ni Mashuti mawili tu ndio yaliyolenga Golini na takwimu hizo zote zinalenga kuonyesha pengo kubwa aliloacha Nahodha wao Robin van Persie alietimkia Manchester United ambae Msimu uliopita aliwafungia Mabao 30 ya Ligi.


Wiki iliyopita wakicheza kwao Uwanja wa Emirates, Arsenal walitoka sare 0-0 na Sunderland katika Mechi yao ya kwanza ya Ligi Msimu huu.


Mechi yao inayofuata ni Anfield na Liverpool Jumapili Septemba 2 mwaka huu.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad