Mabingwa kombe la Afrika Mashariki na Kati Yanga wakutana na mdhamini wa kumbe hilo Rais Kagame Kigali, Rwanda . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, August 24, 2012

Mabingwa kombe la Afrika Mashariki na Kati Yanga wakutana na mdhamini wa kumbe hilo Rais Kagame Kigali, Rwanda .


Mabingwa  wa Afrika Mashariki na Kati, Kagame CUP , Yanga Tanzania  wamekutana na Rais Paul Kagame huko Mjini Kigali, Rwanda ambako leo wataanza Ziara yao rasmi ya Mechi za Kirafiki kwa kucheza na Rayon Sports kwenye Uwanja wa Amahoro.



Yanga ambao wametwaa Kagame CUP  mara mbili mfululizo ambapo Mwenyekiti Yussuf Manji, akiongea mbele ya Rais Kagame, alisema: “Tupo hapa kutoa shukran na tukitambua mchango mkubwa wa Rais Kagame katika kuendeleza Michezo ambacho ni kitu kinachotuunganisha Watu katika eneo hili!”



Wachezaji wa Yanga wakisikiliza kwa makini risala ya mwenyekiti wao.




Kwa upande wake  Rais Kagame ametaka Udhamini wake wa Mashindano ya Kagame Cup uendelee hata kama akistaafu kutoka kwenye siasa.


Rais Kagame alisema: “Si kwa sababu Rwanda ni tajiri ndio maana tumetoa udhamini bali ni alama ya kuimarisha mchango wa michezo na umoja wa Watu wa eneo hili.”


Paul Kagame  na Wachezaji wa Yanga
Rais Kagame wa Rwanda alianza kudhamini Mashindano ya Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati tangu Mwaka 2002 akitoa Dola 60,000 kama zawadi kwa Washindi na Dola 15,000 kama mchango wa kuendesha michuano hiyo na ndio maana Kombi hilo huitwa rasmi Kagame Cup.




Raisi wa Rwanda Paul Kagame akisalimiana na Mama Fatma Karume na Kocha wa Yanga Saintfield  nchini Rwanda.


Aidha Yanga  ikiwa na Wachezaji wawili wa Amavubi, Timu ya Taifa ya Rwanda, Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite, itaondoka Kigali Jumatatu kurejea Dar es Salaam.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad