Klabu ya Soka ya Yanga leo kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam wamefanikiwa kutetea vizuri Taji lao la Klabu Bingwa Afrika ya Mashariki na ya Kati walipoitandika Timu ngumu ya Azam FC bao 2-0 kwenye Fainali na kuendelea kubaki na kombe hilo la KAGAME baada ya kulitwaa Mwaka jana walipowafunga Mahasimu wao wakubwa Simba kwa bao 1-0.
Aidha Wafungaji wa Yanga leo ni Mastraika wao hatari sana, Hamisi Kiiza na Said Bahanuzi, ambao ndio walipachika bao za leo na kila mmoja kufikisha Bao 6 wakifungana na Teddy Etekiama wa Vita Club ya DRC kwa kuwa ndio Wafungaji Bora wa Mashindano haya.
Bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Hamisi Kiiza katika Dakika ya 44 na Said Bahanuzi akapiga Bao la pili katika Dakika ya 90.
![]() |
Mwenyekiti mpya wa Yanga, Yusuf Manji. |
Hakika hii
ni chereko kubwa huko Jangwani kwa Mwenyekiti mpya wa Yanga, Yusuf Manji, na
Kocha wao mpya Tom Saintfient kwani huu ulikuwa ni mtihani wao mkubwa wa kwanza
tangu watwae nyadhifa zao hivi karibuni.
![]() |
Kikosi cha Vita Club ya Congo DR. |
Katika Mechi
ya awali ya kusaka Mshindi wa Tatu, Vita Club ya Congo DR iliifunga APR ya
Rwanda bao 2-1.
No comments:
Post a Comment