![]() |
Mkuu wa Wilaya ya Ngara Bw Constantine Kanyasu wa tatu kulia |
Baadhi ya
wapanda pikipiki wanaofanya kazi ya kubeba abiria katika wilaya ya Ngara mkoani
kagera wamesema wanafanya kazi katika mazingira magumu kutokana na changamoto
ya kukosa leseni kutoka makao makuu ya mkoa.
Wakizungumza
katika mkutano na mkuu wa wilaya Bw Constantine Kanyasu, wapanda pikipiki hao
wamesema kazi yao inakuwa ngumu kwa kukimbizana na polisi kutokana na kufanya
kazi bila leseni.
Mwenyekiti
wa wapanda pikipiki hao Bw Yazzidu Wilsoni amesema kwa sasa wamejiunga katika
vikundi vya kukopeshana ili kupata fedha itakayowawezesha kupata mafunzo na
leseni ambazo upatikanaji wake bado kero.
Hata hivyo
Mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera Bw Costantine Kanyasu ametoa muda wa
miezi miwili kwa madereva wa vyombo vya usafiri wasio na leseni kuhakikisha
wanazitafuta na kuzisajili ili kufanya kazi kwa kuzingatia sheria.
Bw Kanyasu
amesema kwa kutumia umoja wao jeshi la polisi lifanye taratibu za kuwahamasisha
watoa leseni mkoani kufika wilayani Ngara ili kutoa mafunzo Sambamba na leseni
ili waweze kuendesha shughuli kwa kufuata sheria.
No comments:
Post a Comment