![]() |
Jingo la Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) |
Mkazi wa
Kariakoo jijini Dar es Salaam, Ahmad Selemani anashikiliwa na jeshi la Polisi
baada ya mita yake ya Luku kukutwa na yuniti za umeme elfu 29 na 365 zenye
thamani ya shilingi milioni nane.
Meneja wa
Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) Kanda ya Ilala, Athanasius
Nangali, amesema mtu huyo hajawahi kununua umeme tangu alipounganishiwa mita
hiyo mwaka 2010.
Aidha katika
tukio jingine lililotokea eneo la Kariakoo Mtaa wa Magila Meneja wa Hoteli ya
Akubu Paradise, Inocent Masawe amekamatwa akiwa na yuniti elfu moja na mia moja
za umeme kwenye mita yake ya Luku, zenye thamani ya shilingi milioni 4.
Bw Nangali
amesema mteja huyo amekuwa akifanya ujanja wa kununua umeme kidogo kwa ajili ya
matumuzi ya hoteli yake, lakini umeme uliomo kwenye mita ni mwingi kuliko kiasi
anachonunua.
Kufuatia
hatua hiyo ametoa wito kwa watanzania kutoa taarifa za wanaoihujumu TANESCO na
kuahidi kuwa watuhumiwa wote waliokamatwa watafikishwa mahakamani baada ya
upelelezi kukamilika.
No comments:
Post a Comment