 |
Inakadiriwa Watu wapatao billioni 40 kote duniani waliangalia ufunguzi
wa michezo ya Olimpiki katika televisheni.
|
Nchi ya Uingereza
ilifungua michezo ya Olimpiki ya mwaka 2012 Ijumaa kwa mbwembwe za ndege za
kivita zikipita juu ya uwanja, maonyesho ya fataki na halaiki iliyoonyesha
historia ya michezo hiyo kuanzia 1896 mpaka sasa.
Karibu
watazamaji 60,000 walishuhudia mwigizaji aliyevalia kama Malkia Elizabeth
mwenye umri wa miaka 86 akiingia katika uwanja wa Olimpiki kwa parachuti
akifuatana na mcheza sinema za James Bond - Daniel Craig.
Muda mchache
baadaye Malkia mwenyewe alisimama kimya wakati watoto wanaimba wimbo wa taifa
"God Save the Queen".
Baadaye
kidogo gwaride la mataifa lilifuatia huku wanamichezo zaidi ya 10,000 wakiingia
uwanjani na kupita mbele ya jukwaa kuu huku Mataifa 204 yanashiriki katika
michezo ya mwaka huu.
Mashindano
hayo ya siku 17 katika michezo 26 yanaanza Jumamosi na kuendelea mpaka August
17.
 |
Kila la kheri Timu ya Tanzania.
|
Aidha katika
michezo iliyoanza Timu za Soka toka Nchi za Afrika zinazoshiriki Michezo ya
OLIMPIKI LONDON 2012 zimecheza Mechi zake za mwanzo za Makundi na hakuna hata
moja iliyoshinda isipokuwa sare kwa Timu za Gabon, Senegal na Morocco kwa
Wanaume huku Misri ikifungwa bao 3-2 na Brazil na Timu za Wanawake zote
zikifungwa.
Wanawake
walicheza Mechi zao Jumatano July 25
mwaka huu na Banyana Banyana, Timu ya Afrika Kusini, ilipigwa bao 4-1 na Sweden
na wenzao Cameroun walichapwa 5-0 na Brazil.
 |
OLYMPIKI 2012 kutoka LONDON, UINGEREZA ambapo
|
Matokeo kwa
Wanaume Alhamisi Julai 26
Honduras 2
Morocco 2
Gabon 1
Switzerland 1
Britain 1
Senegal 1
Brazil 3
Egypt 2
Matokeo kwa wanawake
Julai 25
Cameroon 0
Brazil 5
Sweden 4
South Africa 1
Mechi zifuatazo ni Jumamosi Julai 28 kwa Wanawake na Wanaume ni Jumapili
Julai 29.
No comments:
Post a Comment