Mgomo wa walimu wafanikiwa katika maeneo mbalimbali nchini - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, July 31, 2012

Mgomo wa walimu wafanikiwa katika maeneo mbalimbali nchini

Shule ya msingi Ruganzo.
Walimu nchini Leo(July 30)mwaka huu  wananza mgomo kuitikia wito wa chama cha walimu nchini CWT ili kuishinikiza serikali kuboresha maslahi yao.
 
 
Uchunguzi  katika maeneo mbalimbali nchni umebaini kuwa walimu wengi wameitikia wito wa kugoma kufanya kazi  huku uchunguzi katika shule za msingi Ruganzo, Ngara mjini ,Nakatunga na kumuyange wilayani Ngara  mkoani Kagera umeonesha kuwa walimu wa shule hizo hawakufika shuleni.
 
 
Mwalimu wa shule ya Sekondari Ntobeye  Bw Sharaza Tadeo amesema hawezi kuingia darasani kwa kile alichokieleza kuwa serikali imeshindwa kutatua kero zao.
 
Katika shule hizo walimu wakuu ndio walioonekana mashuleni huku wanafunzi wakicheza  michezo mbalimbali.
Wilayani Kibondo mkoani Kigoma,Chama cha walimu CWT kimewataka wanachama wake kuunga mkono mgomo ambapo Katibu wa CWT wilayani humo Bw.Lazaro Nkwavu amesema mgomo huo utaendelea hadi hapo Serikali itakapotekeleza madai yao.
 
 
Bw. Nkwavu ameyataja baadhi ya madai yao kuwa ni pamoja na nyongeza ya mshahara kwa asilimia 100,posho ya kufundishia 55% kwa walimu wa masomo ya Sayansi na asilimia 50 kwa wanaofundisha masomo ya sana.
 
 
Katibu huyo ameyataja madai mengine kuwa ni Posho ya kujikimu katika mazingira magumu,na kuwataka walimu kutotishika kwa vitisho vinavyotolewa na baadhi ya maafisa wa Serikali.


Katika hatua nyingine jumla ya wabunge sita wametaka bunge lisitishe shughuli zake ili lijadili mgomo wa walimuu  ulioanza leo.
 
 
Wabunge hao wakiongozwa na mbunge Yahya Kassim Issa wamelitaka bunge kusitisha shughuli zake ili lijadili mgomo huo wa walimu nchi nzima.
 
 
Naibu Spika wa Bunge  Bw Job Ndugai amesema suala hilo haliwezi kujadiliwa kwa kuwa limefikishwa mahakamani.
 
 
Bw Ndugai amesema taarifa alizopatiwa zinaonyesha kuwa serikali pamoja na CWT  wamewalisha hoja zao katika mahakama kuu ambapo kesho (leo)july 31 ,mchana mahakama itaanza kusikiliza madai yao. 
 
Sorce:radiokwizera.com

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad