Mashindano ya OLIMPIKI 2012 Hispania NJE, Brazil, Japan zasonga, ,China na Marekani wanaongoza kwa MEDALI huku Africa ya Kusini ikishinda Medali kwa Africa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, July 31, 2012

Mashindano ya OLIMPIKI 2012 Hispania NJE, Brazil, Japan zasonga, ,China na Marekani wanaongoza kwa MEDALI huku Africa ya Kusini ikishinda Medali kwa Africa.


Timu iliyopewa nafasi kubwa kwenye Michezo ya Olimpiki  LONDON 2012, Hispania  jana ilichapwa bao 1-0 na Honduras na kutupwa nje ya Mashindano huku kwenye Makundi mengine Neymar akiibeba Brazil kutinga Robo Fainali ikiambatana na Japan ambayo iliifunga Morocco  1-0 na Mkongwe Ryan Giggs alipachika bao moja na kuisaidia Team GB kuichapa UAE bao 3-1.
 
 
Hispania  wametolewa nje ya Olimpiki baada ya kupata kipigo cha bao 1-0 mikononi mwa Honduras hiki kikiwa kipigo chao cha pili kufuatia kufungwa 1-0 na Japan kwenye Mechi ya ufunguzi ya Kundi D.
 
 
Hispania wamebakisha Mechi moja ya kukamilisha ratiba na Morocco.
 
 
Katika Mechi nyingine ya Kundi D Japan wao wameingia Robo Fainali baada ya jana kuitungua Morocco bao 1-0.
 
 
 
Nao Senegal waliichapa Uruguay bao 2-0 kwenye Mechi ya Kundi A na kumaliza Mechi wakiwa Mtu 10 baada ya Mchezaji wao Abdoulaye Ba kutolewa kwa Kadi Nyekundu.
 
 
Katika Mechi nyingine ya Kundi A, Wenyeji Team GB waliichapa United Arab Emirates bao 3-1 kwa bao za Ryan Giggs, Scott Sinclair na Daniel Sturridge.


Team GB sasa inahitaji sare tu itakapocheza Mechi yake ya mwisho na Uruguay ili wasonge mbele.
 
 
Nyota wa Brazil, Neymar, aling’ara sana wakati Brazil ilipoichapa Belarus bao 3-1 katika Mechi ya Kundi C na kuiwezesha Brazil kutinga Robo Fainali.
 
 
Neymar alifunga bao la pili kwa frikiki na bao nyingine mbili zilizofungwa na Alexandro Pato na Oscar zilitengenezwa nae.
 
 
Belarus ndio waliotangulia kupata bao katika Dakika ya 8 mfungaji akiwa Renan ambae ni mzaliwa wa Brazil.
 
 
Kwenye Mechi nyingine ya Kundi C, Egypt na New Zealand zilitoka sare bao 1-1.
 
 
Katka Mechi ya Kundi B, Mexico waliichapa Gabon bao 2-0 kwa bao za Dos Santos.
 
 
Aidha mashindano hayo yakiwa yanaendelea,China na Marekani wanaongoza kwa MEDALI huku Africa ya Kusini ikishinda Medali kwa Africa.
 








RankCountry Gold       Silver        Bronze
1 95317
2 57517
3 3137
4 3014
5 2428
6 2226
7 2035
8 2002
9 14611
10 1214
11 1203
12 1113
12 1113
14 1102
15 1023
16 1001
16 1001
16 1001
19 0202
20 0123
21 0101
21 0101
21 0101
21 0101
21 0101
21 0101
27 0011
27 0011
27 0011
27 0011
27 0011
27 0011
27 0011
27 0011
27 0011
27 0011
27 0011
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad