![]() |
Katibu (FAKADI) Denisa Lazaro.
|
Na:Issa
Ngumba Kakonko.
Katibu wa
chama cha soka wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma Denisa Lazaro,amesema hatambui ligi ya jamii
iliyokuwa ikichezwa katika kata ya Kasanda na kusabisha kifo cha mchezaji Inocent Daniel aliyekuwa akichezea
timu ya Kazilamihunda FC ,aliefia uwanjani wakati timu yake ilipokuwa ikichuana
na timu ya Chilambo FC katika uwanja wa Kasanda.
Denisa
amesema kuwa chama cha soka wilaya ya
kakonko (FAKADI) hakitahusika na lolote kuhusina na tatizo hilo lililotokea katika mchezo huo,kwa
kuwa ligi hiyo watu wa kasanda
walishiriki chini ya uongozi wa soka kutoka wilaya ya kibondo.
Aidha amewataka kusimamisha ligi hiyo hadi pale watakapopata maelekezo kutoka
uongozi wa chama cha soka wilaya ya kakonko (FAKADI) na si kuagizwa na uongozi
wa soka wilaya ya kibondo(KDFA).
Katibu huyo
wa FAKADI Denisa amesema kuwa tayari ofisi
yake imepokea fomu za kugombea uongozi katika chama hicho na amewataka wadau kujitokeza kuchukua
fomu hizo na kwamba fomu hizo zitalipiwa ada ya shilingi elfu 30
kwa ngazi ya uongozi na wajumbe shilingi
elfu 20.
No comments:
Post a Comment