Umoja wa
wanamuziki wa Bongo Flava, Rhumba, Dance, muziki wa Injili na aina zingine leo
umetoa agizo kwa makampuni yanayouza miito ya simu nchini pamoja na makampuni
ya simu kuiondoa miitio hiyo ndani ya siku saba kuanzia leo mpaka pale
watakapokubaliana mikataba mipya.
Katika barua
hiyo iliyoandikwa kwenda kwa waandishi wa habari na iliyosainiwa na wasanii
zaidi ya 150 nchini, wasanii hao wameyataka makampuni ya simu kuondoa matangazo
ya ringtone hizo kwenye radio, magazeti, tv, website na kwenye ujumbe mfupi wa
simu.
Hatua hiyo
imechukuliwa na wasanii hao baada ya kubaini kuwa makampuni ya simu
yanawanyonya kwa kiasi kikubwa kwa kuwalipa chini ya asilimia 10 ya mauzo ya
ringtone hizo huku yenyewe yakibaki na zaidi ya asilimia 80.
Wiki
iliyopita mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe aliliibua suala hilo bungeni na kudai
kuwa imeundwa kamati itakayoangalia upya utaratibu wa mauzo ya ringtone.
Press
Release ndio hii.
YAH: KUFUTA
MIKATABA NA KUSIMAMISHA KUUZA MUZIKI WA BONGO FLEVA,GOSPEL,DANSI NA TAARABU
KWENYE MITANDAO YA SIMU.
Husika na
kichwa cha habari hapo juu,
Kwa ujumla
wetu sisi Wasanii toka Tanzania tunaofanya muziki wa Gospel, Rhumba , Taarabu
pamoja na Bongo fleva tumeamua kutoa agzio kwenu la kusimamisha mauzo ya kazi
zetu za muziki katika mtindo wa Ringtone na Callertunes katika mitandao ya simu
ya Vodacom, Zantel,Tigo na Airtel na kufuta mkataba tuliosaini kati yetu sisi
Wasanii na Kampuni yako mpaka hapo tutakapokaa sisi kama wasanii, nyinyi kama
wasambazaji wa muziki wetu, pamoja na Mitandao ya simu ili kuzungumzia namna
mpya ya sisi na nyinyi tutakavyofanya kazi.
Sababu ya
sisi Wasanii kusimamisha na kufuta mikataba kati yetu na wanaofanya biashara ya
kuuza maudhui yetu ni pamoja kampuni husika kushindwa kuweka wazi taarifa za
mauzo ya nyimbo pamoja na kutolipa katika muda husika kama ilivyoanishwa katika
mikataba husika.
Sababu ya
pili ni mitandao ya simu kuchukua kiasi kikubwa cha fedha ambacho ni asilimia
themanini ya mauzo yote ya maudhui yetu, jambo hili linatuumiza na limetufanya
tuendelee kuishi kwa kutegemea aina moja ya pato toka kwenye shoo.
Hivyo
tumeziagiza kampuni zote zinazofanya kazi ya kuuza maudhui yetu kutoa maelekezo
kwenye mtandao husika kuwaelekeza kusimamisha mauzo ya kazi zetu za sanaa ndani
ya siku saba kuanzia leo tarehe 30/07/12 ikiwa pamoja na kusimamisha matangazo
yote yanayotangaza mauzo ya kazi zetu kwa njia ya Television , Radio , blogs,
website, Magazeti na Ujumbe Mfupi wa maneno mpaka hapo tutakapofikia muafaka.
Jumla ya
wasanii 153 wameshasaini barua hizo na wengine wanaendelea kusaini.
Mwisho
tunawashukuru kwa ushirikianao wenu, na tunaambatanisha sahihi zetu ili
kuonyesha uthibitisho wa umoja wetu katika jambo hili.
Asante.
No comments:
Post a Comment