WATAWALA WA KIJESHI WA MALI KUMSHITAKI RAIS AMADOU ALIYEPINDULIWA. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, April 05, 2012

WATAWALA WA KIJESHI WA MALI KUMSHITAKI RAIS AMADOU ALIYEPINDULIWA.

Amadou Sanogo.
Watawala wa kijeshi wanapanga kumfungulia mashtaka ya uhaini rais waliyempindua nchini Mali ambapo Kiongozi wa Mapinduzi Kapten Amadou Sanogo amesema pamoja na mashtaka mengine, Amadou Toumani Toure anakabiliwa na ubadhirifu wa fedha za umma ambapo  imetokea  wakati watawala wa kijeshi wametangaza kuanza kongamano la kitaifa kujadili mustakabali wa nchi ya Mali.


Shirika la Utangazaji BBC wamesema Nchi hiyo ambayo haina bandari, imewekewa vikwazo vya kiuchumi na jamii ya kimataifa ambapo Tangu mapinduzi hayo , waasi wameendelea kuyateka maeneo mengi kaskazini mwa Mali ukiwemo mji wa Timbuktu ambao una hifadhi maalum za kitamaduni na wamegawanyika makundi mawili ambapo lile la MNLA linapigania kuwepo taifa huru la Azawad.Kundi nyingine Ansar Dine lenye uhusiano na mtandao wa Al-Qaeda linataka kusalia Mali lakini chini ya sheria ya Kiisila.

Katika hatua nyingine Sanogo ameliamrisha jeshi lake kusitisha mapigano kaskazini mwa nchi hiyo ambapo amesema ametoa amri hiyo kufuatia waasi wa Tuareg kudhibiti miji ya kaskazini mwa nchi hiyo.
Rais Amadou Toumani Toure
Rais Amadou Toumani Toure alitarajiwa kuondoka madarakani baada ya kumaliza muhula wake wa pili baadaye mwezi huu ambapo katika sentensi nyingine Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kutoa taarifa kuhusu mzozo wa Mali baadaye Jumatano wiki hii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad