Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya kidini Watakiwa kuwania nafasi za uongozi katika vyama vya siasa ili kuimarisha utawala bora katika jamii - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, April 05, 2012

Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya kidini Watakiwa kuwania nafasi za uongozi katika vyama vya siasa ili kuimarisha utawala bora katika jamii

Askofu wa kanisa la Anglikan Dayosisi ya Kagera Dk Aron Kijanjali ametoa wito kwa viongozi wa madhehebu mbalimbali ya kidini kuwania nafasi za uongozi katika vyama vya siasa ili kuimarisha utawala bora katika jamii


Akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu utawala bora, Dk Kijanjali amesema kuwa kiongozi wa dini akipata nafasi ya kuongoza jamii ataongoza katika misingi ya Imani na haki

Amesema kuwa hata watakapokumbwa na changamoto viongozi wa umma ambao pia ni viongozi wa dini wataweza kukabiliana nazo kwa misingi ya haki na usawa kwa kuwa ndani yao tayari wana hofu ya mungu.


Aidha Dk kijanjali amewataka wafuasi wa vyama vya siasa kuepuka rushwa katika changuzi mbalimbali pamoja na kudumisha amani katika chaguzi hizo.

1 comment:

  1. mawazo yake hayo lakin sidhan km yana maana mana hizi din ndo zimekua mstari wa mbele kwa watu kujipatia maslahi.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad