Na: Sylvester Raphael.
Halmashauri
za Wilaya nne Mkoani Kagera zikiongozwa na Halmashauri ya Biharamulo zapata
vyeti vya utoaji huduma bora za afya kwa wananchi katika Hospitali, Vituo vya
Afya na Zahanati kwa kupata nyota kuanzia tatu na kuendelea baada ya tathimini iliyofanywa
na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto mwaka 2017.
Vyeti hivyo
vya huduma bora ya afya vilitolewa na
Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndugulie Julai 28, 2018 Wilayani Muleba ambapo
Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo iliongoza kwa kuwa na nyota nne Katika Hospitali Teule ya Wilaya na Zahanati ya Katoke kwa kupata asilimia
69% pamoja na cheti walipewa ngao ya mshindi wa kwanza.
Wilaya ya Ngara ilishika nafasi ya tatu kwa Hospitali ya Murugwanza kupata nyota
nne na kupata asilimia 51%.
|
Katika
tathmini ya mwaka 2017, wilaya ya Biharamulo imeendelea kushika nafasi ya kwanza, Muleba
ilikuwa ya mwisho kwa tathmini ya mwaka 2016 kwa kutokuwa na kituo chochote
kilichokuwa na nyota tatu lakini kwa mwaka 2017 imeshika nafasi ya pili kimkoa. Aidha, Muleba, Kyerwa, Halmashauri ya Bukoba na Missenyi kwa tathmini ya mwaka 2016 zilikuwa nafasi ya mwisho ambapo hazikuwa na kituo hata kimoja chenye nyota tatu. |
Akitoa vyeti
hivyo Naibu Waziri Dkt. Ndugulile alizipongeza Halmashauri zilizopata ushindi
na kuzisisitiza kuendelea kufanya vizuri ili zifikie nyota tano.
Aidha, Dkt.
Ndugulile alisema kuwa pamoja na ushindi huo lakini hakuna Halmashauri
iliyofikia asilimia 80% kwa hiyo mkoa bado una kazi ya kufanya ili kuhakikisha
kila Halmashauri inafikia kiwango cha kitaifa cha asilimia 80%.
Katika
hautua nyingne Naibu Waziri Dkt. Ndugulile aliagiza Waganga Wakuu wa Wilaya
kuhakikisha wanasimamia Madaktari na Watumishi wa idara ya Afya wanapotoa
huduma kwa mgonjwa katika vituo kila mmoja kwa nafasi yake aandike muda aliomhudumia
mgonjwa ili kuhakikisha mgonjwa anapata huduma kwa wakati na likitokea tatizo
ajulikane ni yupi kafanya uzembe.
Naibu Waziri
Dk. Ndugulile alimalizia hotuba yake fupi kwa kuzitaka Kamati za Ulinzi na
Usalama za Wilaya kuhakikisha zinasimamia dawa za Serikali zenye nembo ya “MSD”
na “GOT”
haziuzwi kwenye maduka binafsi na zikipatikana katika maduka binafsi wahusika
wachukuliwe hatua za kisheria
|
Mkuu wa
Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard
Luyango kwa Niaba ya Serikali alishukuru Wizara ya Afya kwa kuendelea kuboresha
huduma kwa wananchi na kusisitiza kuwa viongozi wote Mkoani Kagera wataendelea
kusimamia ili upatikanaji wa huduma bora zinapatikane na wananchi wapate huduma
bora na kwa wakati.
Mwisho Mkuu
wa Wilaya Luyango aliipongeza Halmashuri ya Wilaya ya Biharamulo kwa kupata
ushindi wa kwanza katika mkoa na kuitaka Halmashauri hiyo kuendelea na uboreshaji
wa huduma ili kuendelea kushika nafasi ya kwanza pia alizitaka Halmashauri
zilizofanya vibaya kwenda kujifunza katika Halmashauri ya Biharamulo ili nazo
ziweze kufanya vizuri.
|
No comments:
Post a Comment