![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhL73risHDTUb5PBdIOlhCpyIrWwecyGG4Vvg9HrIGsYil0ylNJ9gItk8xR94qQDABJauNQQtOwJ9D5S2xhAcXVmUnWAjv1iMGB-Wzt8mXqwE3x0TCVGBiTpX2UIUQXjALwUc3iCePU3nz9/s640/thumb_790_800x420_0_0_auto.jpg)
Halmashauri
ya Wilaya ya Ngara katika kipindi cha Januari hadi Machi 2018, imepokea kiasi
cha shilingi 985,438,660.00 toka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), kwa ajili
ya kutekeleza mpango wa kunusuru kaya masikini (TASAF III).
Mratibu wa
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Bw. Sakina Chamiti, aliyasema hayo Mei
16-17, 2018 wakati wa kikao cha Baraza la waheshimiwa madiwani kilichafanyika
katika ukumbi wa Halmashauri.
“Tulipokea
shilingi 507,224,000.00 ambazo tulizitumia katika kutekeleza uwasilishaji wa
fedha, na kiasi cha shilingi 478,214,660 tulizitumia katika mradi wa kutoa
ajira za muda (PWP) kwa walengwa wetu.” Alisema Bw.Chamiti.
Amesema
katika kipindi cha Januari hadi Februari 2018, Halmashauri ilipokea shilingi
253,796,000.00, ambapo shilingi 253,224,000.00 zimetumika na shilingi
572,000.00 hazijatumika.
Bw.Chamiti amesema katika kipindi cha Machi – Aprili 2018, walipokea shilingi
253,428,000.00, kwa ajili ya kuwalipa walengwa, na kwamba zoezi la kuwalipa
linaendelea.
Aidha, kiasi
cha shilingi 478,214,660 kimepokelewa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kutoa
ajira za muda mfupi (PWP), ambapo kiasi cha shilingi 70,140,700.00 zimetumika
na kuongeza kuwa hadi Aprili 2018 kiasi cha shilingi 191,742,860.00
hazijatumika.
Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii (TASAF) unatoa huduma katika vijiji vipatavyo 56 vilivyomo
katika mpango wa TASAF III, ambapo vijiji 42 vitapata ruzuku ya malipo kwa
walengwa na vijiji 14 vinatarajiwa kuwa katika kundi la utafiti.
No comments:
Post a Comment