Real Madrid
wameweka rekodi mpya Jana May 1, 2018 baada ya kufuzu kwenda Fainali ya UEFA
Champions League 2017/2018 kwa mara ya 16, huku Kocha Zinedine Zidane akiwa
kocha wa kwanza kufuzu kwenda fainali hizo mara 3 mfululizo baada ya Marcelo
Lippi 1996/1998.
Dakika ya 3
tu Joshua Kimmich aliwanyanyua kwenye viti mashabiki wa Bayern Munich baada ya
goli la utangulizi, goli ambalo limemfanya Kimmich kuhusika katika mabao 7 ya
Bayern Munich katika UEFA Champions League msimu huu (kafunga 4 na
assist 3).
|
Goli la
kusawazisha la dakika ya 11 la Karim Benzema limekuwa goli la pili msimu huu wa
Champions League kufungwa baada ya kupigwa pasi nyingi(28), ni bao la Lucas
Digne pekee ndilo ambalo zilipigwa pasi nyingi kuliko hili(29).
Karim
Benzema aliongeza bao la pili dakika ya 46 na hii kuwa mara yake ya kwanza
kufunga mabao 2 katika mechi moja ya Champions League tangu afanye hivyo mara
ya mwisho mwaka 2014 vs Schalke 04.
James
Rodriguez dakika ya 63 aliufanya ubao wa matokeo kusomeka 2-2 na sasa anakuwa
mchezaji wa saba katika historia ya Champions League kuwahi kuifungia pamoja na
kuifunga Real Madrid, sasa Madrid wanafudhu kwa aggregate ya bao 4-3.
Real
Madrid sasa wanasubiri
mshindi wa mchezo wa leo Jumatano May 2, 2018 kati ya AS Roma dhidi ya Liverpool
kufahamu watacheza na yupi fainali.
|
No comments:
Post a Comment