![]() |
Mtalamu akionesha namna ya kuvaa Mavazi maalumu ya kujikinga na Ebola kwa Wadau wa Afya mkoani Kigoma May 16,2018.
Mganga mkuu
wa Mkoa wa Kigoma Dkt.Paul Chaote
amesema Serikali ya mkoa huo kupitia idara ya afya imechukua hatua za awali
katika kukabiliana na maambukizi ya Ugonjwa wa Ebola ulioripotiwa nchi jirani
ya Kongo
Dkt.Chaote amesema hayo katika kikao cha wadau
wa afya ngazi ya mkoa kilichofanyika kwa lengo la kudhibiti uwezekano wa kuenea
kwa maambukizi ya ugonjwa huo.
|
![]() |
Kwa upande
wake Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Generali Mstaafu Emmanuel Maganga amewataka wataalamu wa afya mkoani humo
kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa weledi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu
kwa Wananchi juu ya dalili za awali za ugonjwa huo.
Nchi ya DRC
imekuwa na milipuko mingi ya Ebola kuliko nchi yoyote duniani. Katika
kipindi cha miaka 10 iliyopita kumekuwa na milipuko 5 ambayo ni mwaka 2007,
2008 hadi 2009, 2012, 2014 na 2017.
Kwa taarifa
zilizopo, tayari watu 23 wamefariki kutokana na ugonjwa wa virusi vya Ebola
nchini Congo DRC.
Ebola ni
ugonjwa unaotokea katika kipindi fulani na kuua watu wengi kwa muda mfupi.
|
No comments:
Post a Comment