Seerikali imetakiwa kuzihudumia vyema shule zake na kuboresha mazingira
na miondombinu ya kufundishia ili ziweze kushindana na shule binafsi ambazo
zimekuwa zikifanya vizuri katika mitihani hususan shule za msingi na sekondari.
Hayo yamesemwa na Mbunge wa Kakonko mkoani Kigoma, Kasuku Bilago,
wakati akichangia hoja katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia iliyowasilishwa Bungeni jijini Dodoma ambapo amesma shule za
serikali zimekuwa zikifanya vibaya katika mitihani hiyo, jambo ambalo
litaendelea kudidimiza elimu nchini.
Akiendelea kuchangia bajeti hiyo iliyowasilishwa na Waziri, Profesa. Joyce
Ndalichako, Bilago alisema kwenye shule za binafsi kuna motisha kwa
walimu na mpangilio mzuri wa ufundishaji, jambo ambalo linafanya shule hizo
kufaulisha zaidi ikilinganishwa na shule za serikali ambazo walimu wake wanadai
malimbikizo ya malipo yao, hawana nyumba za kuishi, morali ya kufundisha
imeshuka na mazingira magumu ya kufundishia ikiwemo vitabu, maabara na vifaa
vingine vya nadharia na vitendo.
Aidha, Bilago amedai ‘ugomvi’ kati ya serikali na shule
binafsi ni wivu tu wa serikali kutotaka kushindwa huku akiwataka kuiga mfano na
mifumo inayotumiwa kwenye shule hizo binafsi ili kuinua ufaulu wa wanafunzi.
VIDEO “Hivi Serikali Inawahusu Nini, ni Wivu Tu” – BILAGO |
Tuesday, May 01, 2018
“Hivi Serikali Inawahusu Nini, ni Wivu Tu” – BILAGO
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment