![]() |
Hospitali ya
Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma imepokea vitanda na mashuka vyenye thamani ya
shilingi milioni 5 vilivyotolewa na Benki ya NMB Tawi la Kibondo katika kuunga
mkono utoaji huduma bora ya afya kwa wananchi.
Meneja Kanda
ya Magharibi wa Benki hiyo Bw Leoni
Ngowi akizungumza katika makabidhiano hayo amesema kuwa msaada huo ni
sehemu ya kile ambacho kinachangiwa na Wananchi wa wilaya ya Kibondo kupitia Benki
hiyo.
|
![]() |
Awali
akizungumzia hali ya uhaba wa vitendea kazi katika Hospitali ya wilaya hiyo,
Mganga mkuu wa wilaya ya Kibondo, Dr
Pima Sebastian amesema vitu hivyo vitasaidia wao kutoa huduma kwa ufasaha
ikiwa ni pamoja na kupunguza swala la wagonjwa wawili kutumia kitanda kimoja.
Na –Radio Kwizera KIBONDO.
|

No comments:
Post a Comment