Mkuu wa Mkoa
Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu akizindua zoezi la chanjo ya
saratani ya shingo ya kizazi inayotolewa mkoani humo kuanzia Jana April
23,2018.
|
Wakati wa
zoezi la uzinduzi wa chanjo hiyo ambapo kimkoa imezinduliwa katika Kituo cha
afya cha Kaigara wilayani Muleba,Mkuu wa Mkoa amewataka Wakuu wa Wilaya wote
mkoani humo, kusimamia kwa ukamilifu zoezi hilo kwani linatolewa bure hivyo ni
wajibu wa wazazi na walezi kuhamasisha wasichana kujitokeza kwa wingi.
|
Dalili za
ugonjwa wa Saratani ya Mlango wa Kizazi ni kuishiwa damu, figo kushindwa
kufanya kazi, kuvimba miguu, kutokwa na usaha wa rangi ya kahawia katika sehemu
za siri za mwanamke.
Aidha,
visababishi vya ugonjwa huo ni kuanza mapenzi katika umri mdogo, kuwa na
wapenzi wengi, na kuvuta sigara.
Ili
kujikinga na ugonjwa wa Saratani ya Mlango wa Kizazi ni muhimu sana wasichana
wakazingatia kutojihusisha na visababishi vilivyotajwa hapao juu.
Pia Katika
Mkoa wa Kagera kuna vituo vipatavyo 56 vinavyohusika na uchunguzi wa awali wa
ugonjwa wa Saratani ya Mlango wa Kizazi ambapo mkoa unatoa wito kwaakina mama
kuwahi mapema katika vituo hivyo pale wanapohisi dalili hizo ili kufanyiwa
uchunguzi mapema.
|
No comments:
Post a Comment