Picha/Habari Na Radio Kwizera.
Watoto
wawili wakazi wa kijiji cha Katongo kata ya Rulanda wilaya ya Muleba mkoani
Kagera wamefariki papo hapo baada ya kugongwa na basi wakati wakienda kwenye
masomo ya dini ya kiislamu (madrasa) katika kijiji hicho.
Afisa
mtendaji wa kata ya Rulanda wilayani Muleba Adamu Kamiani aliwataja wanafunzi waliofariki kuwa ni
Muhajiri Abdul Majid (6) na Abdallah Khalid (7) ambao waligongwa leo April 28,
2018 majira ya saa 2:15 asubuhi wakati basi hilo la Kampuni ya Frester lenye
namba za usajili T 720 DEV lililokuwa likitokea Bukoba kuelekea Mwanza likimkwepa
Mwendesha bodaboda na wao kugongwa
wakitembea kwa miguu
Kamiani alisema baada yamajeruhi
kuondoshwa kwenye vyuma vya basi hilo walipelekwa kituo cha Afya Kaigara
na hospitali ya Rubya wilayani Muleba kwa matibabu zaidi.
|
Kwa mujibu
wa abiria waliokuwa kwenye basi hilo wamesema, chanzo cha ajali ni dereva wa
basi alipokuwa akimkwepa mwendesha bodaboda hivyo kuwaparamia vijana hao na
kusababisha basi hilo kupinduka.
Muuguzi wa
zamu wa kituo cha afya Kaigara Monica
Magesa alisema kwamba walipokelewa majeruhi 20 huku wengine saba waliokuwa
na hali mbaya walipelekwa Hospitality ya Rubya kwa matibabu zaidi.
Kamanda wa
Jeshi la polisi mkoani Kagera Agustino Olomi limefika eneo la alithibitisha
vifo vya wanafunzi hao na kwamba jeshi hilo limamshikilia dreva wa basi Mohammed Jafari (49) huku likiendelea
kufanya uchunguzi
Kamanda
Olomi amewataka Madereva kuwa makini wakati huu wa mvua na kuacha
kwenda mwendo kasi unaowafanya kuvunja sheria za usalama barabarani lazima
wafuate utaratibu
|
No comments:
Post a Comment