Mkuu wa Mkoa
wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu amefanya ziara ya siku moja
wilayani Ngara February 5,2018 Kukagua ujenzi wa miradi mitatu ya Kituo vya
Afya Murusagamba kinachofanyiwa upanuzi kwa kujengwa wodi na nyumba za
watumishi ambapo mpaka kukamilika zitatumika Sh Milioni 400, Kituo cha Afya
Mabawe ambacho nacho kinafanyiwa upanuzi wa majengo kikitengewa Sh Milioni 400
na Mabweni ya Sekondari ya Murusagamba ambayo hata Mkuu wa mkoa alikataa
kuyazindua na kuagiza yafanyiwe marekebisho kutokana na kukutwa na mapungufu.
|
Wananchi wa Mabawe wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa
wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu aliyefika Kituo cha Afya Mabawe kukagua ujenzi wa Kituo hicho kinachofanyiwa upanuzi wa majengo ili kuboresha huduma za afya.
|
No comments:
Post a Comment