Rais John Magufuli akiweka taji la
maua katika mazishi ya komredi Kingunge Ngombale Mwiru.
Rais John Magufuli ameongoza waombolezaji katika
mazishi ya Mwanasiasa Mkongwe nchini Kingunge Ngombale Mwiru aliyezikwa kwenye
makaburi ya Kinondoni Jijini Dar Es Salaam shughuli iliyotanguliwa na ibada
iliyofanyika nyumbani kwake kabla ya kuagwa Kitaifa katika Viwanja vya
Karimjee.
Kingunge alikutwa na umauti Siku ya Ijumaa
akiwa anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili baada
ya kushambiliwa na mbwa nyumbani kwake mwezi uliopita jijini, Dar es Salaam.
Shughuli ya
kuaga mwili wa Kingunge iliongozwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na
kuhudhuriwa na Marais Watatu Wastaafu pamoja na viongozi wengine wastaafu
wakiwemo mawaziri wakuu na viongozi wa vyama mbalimbali.
Wasifu wa
Marehemu Kingunge ulisomwa huku Serikali nayo ikitoa salamu zake kupitia kwa
Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo bila kusahau Baraza la Vyama Vya Siasa
likiwakilishwa na Mwenyekiti wake, John Shibuda.
|
No comments:
Post a Comment