Mtibwa Sugar
imefanikiwa kwenda hatua ya 16 Bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup
baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Maji Maji Rangers Uwanja wa
Ilulu mjini Lindi.
Mabao ya
Mtibwa Sugar katika mchezo wa Jana January 31,2018 yamefungwa na mshambuliaji
Kevin Sabato Kongwe kwa mipira ya adhabu, la kwanza dakika ya 36 baada ya
Haruna Chanongo kuangushwa na la pili dakika ya 46 baada ya Salum Kihimbwa
kuangushwa.
Maji Maji
walipata bao la kufutia machozi dakika ya 84 kwa penalti, lililofungwa na Peter
Pole kwa bada ya Issa Kadia Mwanga wa Mtibwa Sugar kuunawa mpira kwenye boksi.
Matokeo ya Mechi
nyingine , Tanzania Prisons imesonga mbele kwa ushindi wa penalti 5-4 baada ya
sare ya 1-1 dhidi ya Burkina FC Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na Maji Maji FC ya Songea imeshinda 2-1 dhidi
ya Ruvu Shooting ya Pwani.
Nayo Njombe
Mji FC imeshinda kwa penalti 4-1 baada ya sare ya 2-2 na Rhino Rangers Uwanja
wa Saba Saba- Njombe, Stand United imeichapa Pamba FC 2-0 Uwanja wa CCM
Kirumba- Mwanza na Kiluvya United imeichapa 2-0 JKT Oljoro Uwanja wa Mabatini
Mlandizi mkoani Pwani.
Mchezo kati
ya Green Warriors na Singida United umemalizika kwa sare ya 0-0 na Singida
kufuzu kwa Penati 4-3 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam,
wakati mechi kati ya KMC na Toto Africans imesogezwa mbele hadi Februari 7,
mwaka huu.
Ikumbukwe
katika mechi za January 30, 2018 Matokeo yake yalikuwa kama ifatavyo hapa
chini.
|
No comments:
Post a Comment