Yanga SC na Azam FC waungana na Buseresere FC na Mbao FC 16 Bora ya Kombe la Shirikisho (ASFC). - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, January 31, 2018

Yanga SC na Azam FC waungana na Buseresere FC na Mbao FC 16 Bora ya Kombe la Shirikisho (ASFC).

Kikosi cha Yanga SC.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Yanga SC imefanikiwa kusonga mbele kwa kuifunga Timu ya Ihefu FC inayoshiriki Ligi daraja la pili goli 4-3  ikiwa ni  changamoto ya mikwaju ya penati baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya goli 1-1.

Ihefu FC ambao walionesha ushindani mkubwa kwenye mchezo huo na ndio waliwatoa Mbeya City katika uwanja huo huo wa Sokoine jijini Mbeya.
 
Yanga SC walionekana kuelemewa kwenye mchezo huo ambapo walikuwa wanaongozwa mpaka dakika ya 90 kabla ya penati ambayo Obrey Chirwa hakufanya ajuzi na kuisawazishia goli hilo lililodumu dakika 60 .

Kwa matokeo hayo Yanga SC wanasonga mbele kwenye hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho (ASFC) wakiungana na klabu ya Buseresere FC na Mbao FC.
Azam FC.

Nacho Kikosi cha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, kimefanikiwa kuchomoza na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya timu ya Shupavu FC mchezo uliyopigwa Mkoani Morogoro.

Waliyokuwa mashujaa katika mchezo huo ni Azam FC ni  Yahya Zayd aliyeanza kuiandikia bao la kwanza timu hiyo, Idd Kipwagile na Paul Peter aliyehitimisha karamu ya magoli kwa kupiga hat trick.
Azam FC imeingia kwenye mchezo huo dhidi ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Pili Tanzania Bara (SDL) ikiwa na kumbukumbu ya kuitoa Area C United ya Dodoma kwa mabao 4-0, yaliyofungwa na kiungo Salmin Hoza, Nahodha Msaidizi Agrey Moris, Yahya Zayd na Enock Atta.

Michuano hiyo ya Azam Sports Federation Cup ina umuhimu mkubwa kwa kila timu inayoshiriki kwakuwa mshindi huiwakilisha nchi katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad