![]() |
Waziri wa
Nishati wa Tanzania, Dr Medard Kalemani amewaagiza Viongozi wa Mkoa na Wilaya za Kakonko na Kibondo sambamba na Meneja
wa Shirika la Ugavi wa Umeme TANESCO kwenye wilaya hizo mkoani Kigoma kusimamia
miradi ya umeme ya REA awamu ya tatu kwenye maeneo yao ili kutimiza malengo ya
serikali.
Dr Kalemani
ametoa agizo hilo wakati wa uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini (REA) awamu ya
tatu Mkoani Kigoma, uzinduzi ambao umefanyika kwenye kijiji cha Mabamba
Wilayani Kibondo.
|
![]() |
Amesema Serikali imetenga Shilingi Bilioni 60 kwa Miradi ya Umeme kwa Mkoa mzima wa
Kigoma ambapo shilingi Bilioni 25 zimetengwa kwa wilaya za Kibondo na Kakonko
hivyo viongozi hao wanapaswa kuwasimamia wakandarasi kuhakikisha wanafanya kazi
kwa wakati.
Kwa upande
wake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Generali Mstaafu Emmanuel Maganga
amemuhakikishia waziri Kalemani kuwa ofisi yake itasimamia miradi hiyo kwa
karibu huku akiwahimiza viongozi wa wilaya ya Kibondo kuwasimamia wakandarasi
kwenye maeneo yao ili kutimiza malengo ya serikali ya kuwafikishia maendeleo
wananchi.
|

No comments:
Post a Comment