
Bendi ya
muziki nchini Tanzania ya Msondo Ngoma, imemtaka msanii wa muziki wa bongo
fleva, Diamond Platinumz pamoja na kundi lake la Wasafi Classic Baby (WCB)
liwalipe fidia kwa kuiga kionjo cha muziki uliopigwa katika nyimbo ya ‘Ajali’
bila idhini ya mmiliki.
Msondo Ngoma
kupitia kampuni ya Mawakili ya Maxim imeitaka Wasafi Clasic Baby (WCB) kuwalipa
fidia ya kiasi cha shilingi 300 milioni kutokana na kutumia kionjo hicho cha
muziki kilichotungwa na kupigwa katika wimbo wao wa ‘Ajali’ na kukirudia katika
wimbo wao wa ‘Zilipendwa’ bila kupata idhini ya mmiliki.
Kionjo hicho
kilichotungwa na kupigwa kuanzia dakika ya 6:38 hadi 6:52 kwenye wimbo wa
‘Ajali’ mali ya Msondo Ngoma, kimeigwa na kupigwa katika wimbo wa ‘Zilipendwa’
kuanzia dakika ya 4:55 hadi 5:10.
Barua hiyo
imeitaka WCB kulipa fedha hizo ndani ya muda wa siku saba na kama wakishindwa
basi Msondo Ngoma watawachukulia hatua zaidi za kisheria.







No comments:
Post a Comment