
Serikali
ya Tanzania inatarajia kuanzisha mfumo mpya wa Elimu hapa nchini ambao elimu ya msingi
itakuwa inatolewa kwa miaka 6, tofauti na ilivyo sasa ambapo hutolewa kwa miaka
7.
Akijibu
swali linalohusu watoto wa kike kuolewa wakiwa na cheti cha kuhitimu elimu ya
sekondari, Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Joseph Kakunda ametolea
ufafanuzi suala hilo na kusema kwamba mfumo huo mpya utatoa fursa kwa wanafunzi
wa elimu ya msingi kusoma miaka 6, huku chekechea ukiwa ni mwaka mmoja na
sekondari ni maka minne, ambayo itakuwa ni lazima.
“Napenda
kutoa majibu sahihi waliopata mkanganyiko, nilisema sera mpya ya elimu huko
tunakoelekea inabadilisha mfumo wa sasa wa elimu ambao utahitaji mtoto aanze
chekechea mwaka mmoja, elimu ya msingi miaka 6, sekondari miaka minne na
itakuwa ni lazima”, amesema Mheshimiwa Kakunda.
Mheshimiwa
Kakunda ameendelea kwa kueleza kwamba kutokana na mfumo huo mpya ambao
utaruhusu mwanafunzi kusoma kwa muda mfupi, na baada ya kuhitimu ndio utakuwa
kithibitisho pekee kwamba binti amemaliza elimu ya sekondari na ndipo
ataruhusiwa kuolewa.
Hivi
karibuni Waziri kakunda alitoa taarifa ikisema kwamba ili mtoto wa kike aweze
kuolewa atahitaji kuwa na cheti cha kuhitimu sekondari, suala ambalo liliibua
mjadala kwa wananchi.





No comments:
Post a Comment