![]() |
|
Mganga mkuu
wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera ,Dr Revocatus Ndyekobora amesema Majeruhi 33 kati ya 44 waliojeruhiwa kwa bomu la kutupwa kwa mkono Novemba 8,2017 wameruhusiwa
kutoka hospitalini baada ya afya zao kuimarika.
Aidha amesema
Majeruhi 11 wamefanyiwa kipimo cha X Ray
na Madaktari Bingwa kutoka Bugando/Mwanza na Hospitali ya Mkoa wa Kagera na kwamba wamewabaini kukutwa na vyuma ndani ya miili yao hivyo wataendelea kuchunguzwa
zaidi kubaini kama vyuma vilivyomo
vinahitaji kutolewa ama la na kupatiwa matibabu zaidi.
|
![]() |
|
Mkuu wa wilaya
Ngara Luteni Kanali Michael Mtenjele.
November
8,2017 Majira ya asubuhi ,Wanafunzi wa Tano
wa darasa la kwanza wa Shule ya msingi Kihinga,iliyopo wilayani Ngara mkoani Kagera walifariki dunia na wengine 42
na mwalimu wao mmoja kujeruhiwa baada ya kulipukiwa na bomu la kutupwa kwa
mkono na kukimbizwa katika Hospitali ya misheni Rulenge kwa
matibabu zaidi.
Msaada mkubwa unahitajika hasa wa - CHAKULA,
MASHUKA/BLANKETI 50,MAFUTA KWA AJILI YA KUSAIDIA KUSAFIRISHA MAJERUHI
WANAOHITAJI RUFAA KWENDA HOSPITALI NYINGINE PAMOJA NA DAMU SALAMA.
MSAADA WAKO
WAWEZA UPELEKA MOJA KWA MOJA HOSPITALI YA MISSION RULENGE AU OFISI YA KATIBU
TAWALA WILAYA YA NGARA.
TUENDELEZE
KWA VITENDO UTAMADUNI WA UZALENDO WA KUSAIDIANA WAKATI WA MAAFA.
|

![]() |
|
Kufatia tukio hilo, Mkuu wa wilaya
Ngara Luteni Kanali Michael Mtenjele (Aliyeweka mkono mfukoni) amepiga marufuku kuanzia sasa kwa Wananchi kufanya biashara ya vyuma
chakavu wilayani humo na kila anayetaka
kufanya shuguli hiyo ajisajili kwa kupata kibali lakini sio kuhusisha wanafunzi wa shule
za msingi na sekondari.
Akiwa katika Hospitali ya Misheni ya Rulenge kuwajulia hali majeruhi alisema mbele ya
wataalamu wa afya na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama kwamba yeyote atakayetangaza biashara ya vyuma
chakavu atashughulikiwa na vyombo vya dola.
|









No comments:
Post a Comment