Bodaboda Rulenge/Ngara wajitokeza Kuchangia Damu Salama Majeruhi wa Bomu Kihinga. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, November 09, 2017

Bodaboda Rulenge/Ngara wajitokeza Kuchangia Damu Salama Majeruhi wa Bomu Kihinga.

Umoja wa Wapanda Pikipiki  marufu Bodaboda katika mamlaka ya mji mdogo wa Rulenge wilaya ya Ngara mkoani  Kagera wamejitokeza  leo November 9, 2017 kutoa msaada wa Damu Salama ili kusaidia Majeruhi  43 waliolazwa katika Hospitali ya Kristo Mfalme ya Rulenge baada ya  ajali ya kulipukiwa bomu la mkono wakiwa  shule ya msingi kihinga wilayani humo.

Kiongozi wa Bodaboda, Bw.  Agustine Karoli  amesema  pamoja na kutoa damu  pia walichangia Sh20, 000 kuweza kunua  maji ya kunywa na kwamba wanazidi kuhamasishana kusaidia wanafunzi hao wa darasa la kwanza waliojeruhiwa na ambao ni tegemeo lijaro la Taifa.


Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara Bw.Aidan Bahama amesema kwamba Serikali ya wilaya inatoa  shilingi Milioni 1 kwa ajili ya huduma ya kupata vyakula na huduma nyinginezo zinazohitajika.

Amesema kwa kushirikiana na Kamati ya Maafa ya wilaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama wanafanya kila jitihada kusaidia wanafunzi hao kwa mahitaji ya aina yoyote sambamba na  kuwatia matumaini wazazi wao.

Mkuu  wa wilaya  Ngara Luteni Kanali Michael Mtenjele amezidi kusisitiza  kwa Wananchi kuwa   ni marufuku   kufanya biashara ya vyuma chakavu wilayani humo   na kila anayetaka kufanya shuguli  hiyo   ajisajili kwa kupata kibali  lakini sio kuhusisha wanafunzi wa shule za  msingi na sekondari.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad