|
Timu ya
Taifa ya Tanzania ,Taifa Stars imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na
wenyeji Benin katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa l'Amitie, au Urafiki
mjini Cotonou leo November 12, 2017.
Katika mchezo huo, hadi mapumziko wenyeji The Squirrels, walikuwa mbele kwa bao
1-0.
Bao hilo lilifungwa kwa penalti na mkongwe mwenye umri wa miaka 33, Nahodha,
Stephane Sessegnon anayechezea klabu ya Montpellier ya Ufaransa.
Sessegnon
akamtungua kipa namba moja wa Tanzania, Aishi Manula kufunga bao lake la 21
timu ya taifa katika mechi ya 68.
Tanzania ilisawazisha
kupitia mshambuliaji wa zamani wa Simba
SC ya Tanzania na Dhofar SC ya Oman, Elias Maguri aliyefunga bao hilo
akimalizia krosi ya winga Shiza Kichuya kutoka upande wa kushoto.
Matokeo haya yana maanisha Benin imeshindwa kulipa kisasi cha kufungwa na Tanzania,
kwani mara ya mwisho, zilipokutana Oktoba 12, mwaka 2014 Taifa Stars ilishinda mabao 4-1, mabao ya Nahodha wa wakati huo,
beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ dakika ya 16, kiungo Amri Kiemba dakika ya 39,
Thomas Ulimwengu dakika ya 49 na Juma Luizio, wakati la Benin lilifungwa na
Suanon Fadel dakika ya 90.
|
No comments:
Post a Comment