Kifo cha Kanumba -Mahakama yamhukumu 'Lulu' Miaka 2. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, November 13, 2017

Kifo cha Kanumba -Mahakama yamhukumu 'Lulu' Miaka 2.

Muigizaji Elizabeth Michale, maarufu kama 'Lulu.

Mahakama Kuu ya Tanzania imemhukumu kifungo cha miaka miwili, mwigizaji wa kike, Elizabeth Michael ‘Lulu’ baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake, Steven Kanumba.

Akisoma hukumu hiyo leo November 13,2017, Jaji Sam Rumanyika amesema kwamba ushahidi wa mazingira umemtia kwenye hatia ya kuua msanii huyo, hivyo atatumikia kifungo cha miaka miwili jela.

Lulu alidaiwa kumuua Kanumba Aprili 7, mwaka 2012 eneo la Sinza, Vatican mjini Dar es Salaam.

Marehemu Steven Kanumba alifariki majira ya saa nane usiku,mnamo mwaka 2012 baada ya kutokea mzozo kati yake yake na Elizabeth Michael ambaye inaaminika kuwa walikuwa na uhusiano wa Kimapenzi.

Kanumba, ambaye alijizolea umaarufu mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati na hadi Afrika Magharibi baada ya kuwashirikisha katika filamu zake baadhi ya wasanii maarufu wa kutoka Nigeria akiwemo Mercy Johnson na Noah Ramsey.

Marehemu ambaye alizaliwa mwaka 1984, alianza kujipatia umaarufu mwanzoni mwa mwaka 2000 wakati huo akiigiza katika michezo ya runinga kupitia kundi la maigizo la Kaole Sanaa.
Aliendelea na kuigiza filamu nyingi ambazo zilimpatia umaarufu mkubwa kiasi cha kusafiri mara kadhaa nchi za nje, ambako alitambulika kama mmoja wa wasanii wenye vipaji vikubwa ambaye aliitangaza fani ya filamu nchini Tanzania maarufu kama 'Bongo Movies.'

Mazishi yake yalichukua sura ya kitaifa kutokana na umaarufu aliojijengea msanii huyo katika jamii ya watanzania na hata nchi za nje.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad