![]() |
|
Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea taarifa kutoka
Shirika la Afya Duniani (WHO), mnamo tarehe 19 Oktoba 2017 kuhusu ugonjwa wa
Marburg ambao umejitokeza katika nchi jirani ya Uganda tangu tarehe 17 Octoba,
2017.
Maeneo yaliyoathirika na ugonjwa huo ni Wilaya ya Kween, Kanda ya
Mashariki ya nchi, ambayo inapakana n nchi ya Kenya.
Hadi
kufikia tarehe 19 Oktoba 2017, watu 4 walikwishapata maambukizo ya
ugonjwa huo, ambapo wawili kati yao wamepoteza maisha.
Wizara
inatoa tahadhari ya Ugonjwa huu kwa wananchi katika mikoa yote ya
Tanzania, hususan kwa wale wanaoishi katika mikoa ambayo inapakana na na
nchi ya Uganda (Mikoa ya Mara, Mwanza na Kagera).
Ugonjwa wa
Marburg unafanana sana na ugonjwa wa Ebola.
Virusi vinavyosababisha
ugonjwa wa Marburg vinajulikana kama “Marburg Virus”, navyo vipo katika
jamii moja na virusi vinavyosababisha Ebola (Ebola virus).
Ugonjwa huu ni
miongoni mwa magonjwa yajulikanayo kwa ujumla kama Homa za Virusi zinazosababisha
kutokwa damu mwilini, (Viral Haemorrhagic Fevers). Ugonjwa huu hauna tiba wala
chanjo.
Dalili kuu
za ugonjwa huu ambazo huanza ghafla ni pamoja na Homa kali, maumivu makali ya
kichwa pamoja na mwili kuishiwa nguvu ambapo baadaye huambatana na kuharisha sana
(majimaji), maumivu ya tumbo, kichefuchefu na kutapika na kutokwa damu katika
matundu yote ya mwili yaani pua, njia ya haja kubwa na ndogo, mdomoni,
masikioni, machoni, hali inayopelekea kifo kwa muda mfupi.
Kipindi cha
kuonekana kwa dalili za ugonjwa ni kati ya siku 3 hadi 9 baada ya kupata
maambukizi.
Ugonjwa huu
unaenea kwa urahisi sana na haraka kutoka mtu mmoja hadi mtu mwingine iwapo
mtu atakuwa karibu na mgonjwa na kugusana na mate, damu, mkojo, machozi,
kamasi, maji maji mengine ya mwili, ikiwa ni pamoja na jasho au kumgusa
mtu aliyekufa kwa ugonjwa wa Marburg.
Ugonjwa huu pia unaweza kuenezwa iwapo
mtu atagusa nguo au mashuka ya mgonjwa wa Marburg.
Wizara ya
Afya , imechukua hatua zifuatazo katika kukabiliana na tishio la ugonjwa huu:
Kutoa
taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huu kwa Waganga Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya
kupitia OR-TAMISEMI.
Taarifa hiyo imejumuisha namna Ukweli kuhusu ugonjwa
(Fact sheet),
Kuimarisha
ufuatiliaji wa ugonjwa huu kupitia kwa Wataalamu wa Afya katika Mikoa, Wilaya
na maeneo ya mipaka ya nchi kavu na maji.
Aidha watalaamu hawa wa Afya pia
wanatoa elimu kwa wananchi kuhusu dalili za ugonjwa huu ili endapo ugonjwa huo
utatokea uweze kutolewa taarifa mapema na kushughulikiwa.
Vifaa kinga
kwa ajili ya watumishi wa afya na vipima joto maalum (thermoscan) tayari vipo
katika maeneo husika ya mikoa.
Wananchi
wanashauriwa kutokuwa na hofu kwani hadi sasa hakuna mgonjwa yeyote wa
Marburg aliyeripotiwa nchini.
Wananchi wanashauriwa kutoa taarifa kwenye kituo
cha huduma za afya kilicho karibu mara watakapoona mgonjwa yeyote atakayehisiwa
kuwa na dalili za ugonjwa huu.
Kitengo cha
mawasiliano ya Serikali
30/10/2017
|
Tuesday, October 31, 2017
Wizara ya Afya ya Tanzania yatoa Tahadhali ya Ugonjwa wa Marburg.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.






No comments:
Post a Comment