![]() |
|
Mbunge wa
jimbo la Mtama kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye amefunguka na kuweka sawa
kuwa siku ya kesho Oktoba 31, 2017 hatakuwa na mkutano wowote na vyombo vya
habari na kusema kuwa watu wanatunga hizo taarifa.
Nape Nnauye
ametoa kauli hiyo kupitia mtandao wake wa kijamii na kuwataka watu waache
kumzushia mambo wakiwa na lengo la kutafuta nafasi na vyeo serikalini.
"Acheni kupiga ramli juu ya kesho
yangu!! Kisa mnatafuta vyeo na hamuwezi kutumia akili kufikiri! Sina 'press
conference' kesho" aliandika Nape Nnauye
|
Monday, October 30, 2017
Nape Nnauye -"Acheni kupiga ramli juu ya kesho yangu!!
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.






No comments:
Post a Comment